ULIMBWENDE: Tumia viazi kulainisha ngozi
Na MARGARET MAINA
VIAZI vina madini muhimu kama vitamini A, B, C na chuma na pia vina manufaa kwa ngozi yetu.
Unaweza kutumia viazi nyumbani ili kuwa na ngozi nyororo.
Faida za viazi kwa ngozi
Viazi huondoa madhara yaliyosababishwa na jua na kuleta mwanga wa asili wa ngozi.
Viazi inapunguza uwekundu na matatizo ya ngozi kutokana na vipele ,makovu na chunusi.
Viazi vinafanya ngozi iwe rangi moja na laini.
Viazi husaidia kuondoa mikunjo kwenye uso
Viazi huondoa weusi kwapani
Husaidia ngozi iwe na rangi moja.
Utahitaji
- vijiko vitatu vya juisi ya viazi
- mafuta ya lozi vijiko viwili (almond oil)
- maziwa vijiko viwili
Cha kufanya
Kwenye kibakuli changanya mahitaji yote na upake kwenye uso bila ya kusahau shingo na sehemu zote utakazohitaji.
Iache kwa dakika 30 kisha osha kwa maji fufutende.
Kuondoa makovu na madoa
Mahitaji
- kipande cha kiazi
- sukari vijiko 2
Cha kufanya
Nyunyiza sukari kidogo kwenye kipande cha kiazi na ujisugue kwa dakika tano.
Uache mchanganyiko kwenye uso wako kwa dakika 10 kisha osha kwa maji ya baridi.
Limau na viazi vinatumika kama mkorogo wa asili na huondoa weusi wowote na madoa kwenye ngozi.
Mahitaji
- kiazi kidogo kimoja kilichopondwa
- vijiko vitatu vya juisi ya ndimu au limau
Cha kufanya
Ponda kiazi na eka vijiko vitatu vya juisi ya limau
Changanya na paka kwenye makovu
Iache kama dakika 20 mpaka 30 kisha osha vizuri na maji
Kwa ngozi iliyoungua kutokana na jua
Maji ya viazi yatasaidia ngozi yako
Mahitaji
- vijiko viwili vya juisi/maji ya viazi
- kijiko kimoja cha asali
Cha kufanya
Changanya bidhaa zote unazohitaji pamoja na upake kwenye uso.
Ache kama dakika 15 kisha osha.
Kausha vizuri na paka losheni au mafuta unayopenda.
Kwa kuondoa mikunjo
Viazi huondoa na kupunguza mikunjo kwenye uso
Mahitaji
- kiazi kimoja kilichopondwa
- vijiko viwili vya maziwa
- glycerine kiasi
Cha kufanya
Katika bakuli tia kiazi kilichopondwa na maziwa, changanya vizuri.
Ongeza gycrerine na changanya.
Paka mchanganyiko kwenye uso wako na uache kama dakika 15.
Osha kwa maji fufutende kisha ufute uso.