TUZO ZA KPL 2018: Orodha nzima ya wachezaji watakaomenyana
Na GEOFFREY ANENE
MSHAMBULIAJI Eric Kapaito ametiwa katika vitengo vinne kwenye orodha ya wawaniaji wa tuzo za Kampuni inayoendesha Ligi Kuu ya Soka ya Kenya (KPL) zitakazofanyika Oktoba 25, 2018 katika taasisi ya Kenya School of Government mtaani Kabete viungani mwa jiji la Nairobi.
Kapaito, ambaye klabu yake ni Kariobangi Sharks, alifunga mabao 17 kwenye Ligi ya mwaka 2018 na kuibuka mfungaji bora. Atawania taji la Mchezaji Bora wa Mwaka (Sh1, 000,000), mfungaji bora (Sh500, 000), Mchezaji mwenye nidhamu (Sh200, 000) na Mchezaji mpya wa mwaka (Sh200, 000).
Mwaka 2017, Michael Madoya alishinda vitengo vya Mchezaji Bora wa Mwaka, Mchezaji mpya wa mwaka, Kiungo Bora wa Mwaka na Mchezaji mwenye nidhamu.
Madoya kutoka klabu ya Zoo mjini Kericho ameorodheshwa katika orodha ya wawaniaji wa mataji ya Mchezaji Bora wa Mwaka, Kiungo wa Mwaka na mchezaji mwenye nidhamu.
Patrick Matasi, ambaye amejitokeza kuwa kipa nambari mmoja wa Kenya chini ya kocha Sebastien Migne, yumo mbio kuwania taji la kipa bora wa mwaka kwa mwaka wa tatu mfululizo.
Matasi alishinda mataji ya mwaka 2016 na 2017. Mwaka huu, anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Farouk Shikalo anayechezea Bandari.
Muingereza Dylan Kerr, ambaye mwezi Juni/Julai mwaka 2018 wakati wa mashindano ya Afrika Mashariki na Kati alipigwa marufuku na Shirkisho la Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kwa utovu wa nidhamu, yuko katika orodha ya wawaniaji wa taji la Kocha Bora wa Mwaka. Mkufunzi William Muluya wa Kariobangi Sharks alitwaa taji hili mwaka 2017.
Vita huenda vikali vikali baina ya makocha hawa wawili, ingawa Bernard Mwalala anaweza kuwaharibia sherehe zao hasa baada ya kufanya kazi nzuri akiwa Nzoia Sugar kabla ya kujiunga na Bandari ambako pia alifanya kazi nzuri sana.
Isipokuwa vitengo vya mchezaji bora wa mwaka na tuzo kutoka mwenyekiti wa klabu za Ligi Kuu, washindi wa nafasi tatu za kwanza katika vitengo vingine vyote watazawadiwa fedha. Wadhamini wa Ligi Kuu, kampuni ya bahati nasibu ya SportPesa, imetanga Sh6.75 milioni kama zawadi kwa washindi.
Hivi hapa vitengo vyote na wawaniaji wa vitengo hivyo:
Mchezaji bora wa mwaka (MVP)
Eric Kapaito (Kariobangi Sharks)
Michael Madoya (Zoo Kericho)
Farouk Shikalo (Bandari)
Cliff Nyakeya (Mathare United)
Felly Mulumba (Bandari)
Kipa bora wa mwaka
Farouk Shikalo (Bandari)
Patrick Matasi (Tusker)
Kelvin Omondi (SoNy Sugar)
Mathias Kigonya (Sofapaka)
Ezekiel Owade (AFC Leopards)
Beki wa mwaka
Felly Mulumba (Bandari)
Titus Achesa (Posta Rangers)
Oliver Ruto (Ulinzi Stars)
Haron Shakava (Gor Mahia)
Joash Onyango (Gor Mahia)
Kiungo wa mwaka
Cliff Nyakeya (Mathare United)
Michael Madoya (Zoo Kericho)
Elvis Nandwa (Ulinzi Stars)
Marvin Nabwire (AFC Leopards)
Whyvonne Isuza (AFC Leopards)
Mchezaji mpya wa mwaka
Eric Kapaito (Kariobangi Sharks)
Pistone Mutamba (Sofapaka)
Dennis Boge (Vihiga United)
Amos Kigadi (Vihiga United)
Marvin Nabwire (AFC Leopards)
Mchezaji mwenye nidhamu
Michael Madoya (Zoo Kericho)
Eric Kapaito (Kariobangi Sharks)
Felly Mulumba (Bandari)
Pistone Mutamba (Sofapaka)
Dennis Boge (Vihiga United)
Kocha wa mwaka
Dylan Kerr (Gor Mahia)
Bernard Mwalala (Bandari)
Robert Matano (Tusker)
Danstan Nyaudo (Ulinzi Stars)
John Baraza (Sofapaka)
Meneja wa Timu wa mwaka
Francis Onywera (Kariobangi Sharks)
Vincent Okello (Mathare United)
Emmanuel Geno (Sony Sugar)
Christopher Ouma (Ulinzi Stars)
Lazarus Yogo (Zoo Kericho)
Mfungaji bora wa mwaka
Eric Kapaito (Kariobangi Sharks)
Elvis Rupia (Nzoia Sugar)
Jacques Tuyisenge (Gor Mahia)
Klabu ilioonyesha nidhamu ya hali ya juu
Gor Mahia
Sofapaka
Kariobangi Sharks
Refa wa kupuliza kipenga aliyeimarika zaidi
Davies Omweno (Makanika/Dereva wa lori)
Raymond Onyango (Afisa wa michezo)
Yasin Badr (Dereva)
Andrew Juma (Mwanahabari)
Israel Mpaima (Afisa wa masuala ya fedha)
Refa wa kunyanyua kibendera aliyeimarika zaidi
Gilbert Cheruiyot (mwalimu)
Maryann Njoroge (mfanyibishara)
Tonny Kidiya (mwalimu)
Stephen Yembe (Mtaalamu wa masuala ya kidijitali)
Oliver Odhiambo (afisa wa kulinda wanayama pori)