Habari Mseto

Wanafunzi watia fora kwenye utengenezaji wa vifaa vya teknolojia

Na LAWRENCE ONGARO September 2nd, 2024 1 min read

WANAFUNZI kadhaa wa Chuo Kikuu cha Zetech, kilichoko eneo la Mangu, Kaunti ya Kiambu Jumatatu, Septemba 2, 2024 waling’aa katika mashindo ya utengenezaji wa vifaa vya kiteknolojia.

Mburu Karanja na Simon Wafula walitia fora katika mashindano hayo, kwa jina “World Skill Global Competition” kwa kuvumbua teknolojia ya kuzuia udukuzi wa mitambo ya kompyuta.

Mashindano hayo yalifanyika katika chuo cha kiufundi nchini, Kenya School of TVET, kilichoko jijini Nairobi.

Wanafunzi wengine wa Chuo cha Zetech waliong’aa ni; Kennedy Kimari, Francis Ng’ang’a na Michael Kamau aliyebuni mtambo wa kuchuja maji kuwa safi kupitia njia ya kiteknolojia.

Francis Ng’ang’a mwanafunzi wa Zetech akionyesha ubunifu wake wa kiteknolojia kwa baadhi ya wageni waliohudhuria mashindano ya kiteknolojia ya masomo ya TVET. PICHA|LAWRENCE ONGARO

Msaidizi wa Naibu Chansela katika chuo hicho Prof Alice Njuguna, alipongeza juhudi za wanafunzi hao ya kuweka Zetech katika ramani ya ulimwengu katika nyanja ya teknolojia.

Mashindano hayo yalishirikisha vyuo vya kiufundi nchini huku wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali wakionyesha ubunifu wao katika fani mbalimbali