• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 2:07 PM
Wanjigi aachiliwa bila kushtakiwa

Wanjigi aachiliwa bila kushtakiwa

Na RICHARD MUNGUTI

MWANASIASA Jimi Wanjigi aliyetiwa nguvuni Jumanne usiku na kulala ndani sasa anawalaumu wapinzani wake wa siasa.

Hata hivyo Wanjigi aliyefikishwa mahakamani Jumatano aliachiliwa bila kufunguliwa mashtaka ya ulaghai wa shamba lenye thamani ya Sh56milioni.

Kushtakiwa kwa Bw Wanjigi na mkewe Irene Nzisa kulizimwa na mahakama kuu.

Kiongozi wa mashtaka Bi Everlyne Onuonga alithibitisha agizo hilo la mahakama na kueleza korti, “hatuwezi kuendelea na kesi hii. Tutakuwa tunaidharau mahakama.”

Bi Onuonga alisema mbali na agizo la Jaji Mrima kulikuwa na agizo Bw Wanjigi akamatwe na kushtakiwa.

Hakimu mwandamizi Bw Bernard Ochoi alifutilia mbali agizo hilo la kukamatwa kwa Bw Wanjigi na mkewe Irene.

Lakini agizo washukiwa wengine sita walioagizwa wafike kortini Januari 24,2022 kujibu mashtaka lingalipo.

Baada ya kuzuiliwa kwa masaa tisa katika seli za mahakama ya Milimani Nairobi, Bw Wanjigi aliachiliwa kufuatia agizo la mahakama kuu asishtakiwe.

Akiwahutubia wanahabari Bw Wanjigi alisema ataendelea na azma yake ya kuwania urais kwa tikiti ya chama cha ODM.

Alidai kinara wa ODM Raila Odinga ni mnafiki na msaliti kwa vile hakushauriana na wafuasi wa chama hicho kabla ya handisheki na Rais Uhuru Kenyatta.

“Kulingana na mimi Bw Odinga ni msaliti wa wafuasi sugu wa ODM. Hakupata maoni yao kabla ya handisheki na Rais Kenyatta,”Bw Wanjigi aliwaambia wanahabari.

Bw Wanjigi alisema uteuzi wapasa kufanywa ili ODM imteue mwaniaji wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9,2022.

“Sitafifia wala kusinzia nitasonga na ndoto yangu hadi debeni ya urais.ODM itafanya mkutano wa wajumbe na kumteua mwaniaji wake wa urais. Bw Odinga yuko na azimio,”alisema Bw Wanjigi katika mahakama ya Milimani alipoachiliwa kutoka seli.

Alipuuza Azimio la Umoja akisema ni azma ya mtu mmoja tu.

 

  • Tags

You can share this post!

CHARLES WASONGA: Serikali itwae bunduki haramu North Rift...

Wabunge wa Tangatanga wasema hawaogopi kupokonywa nafasi...

T L