Mshtuko, simanzi mwanafunzi akijiua shuleni
MSHTUKO na huzuni ulikumba Shule ya Wasichana ya Sironga Kaunti ya Nyamira baada ya mwanafunzi wa Kidato cha Nne kuripotiwa kujiua.
Msichana huyo ambaye alikuwa miongoni mwa wale wanaojiandaa kwa mtihani wa KCSE mwezi ujao aliruka kutoka orofa ya tatu ya jengo la ofisi za shule hiyo.
Kisa hicho kilichotokea saa tano asubuhi Jumamosi kilitumbukiza shule ya pekee ya kitaifa ya wasichana Kaunti ya Nyamira katika simanzi huku wanafunzi na walimu wakishangazwa na tukio hilo.
Mkuu wa shule Jane Nyanumba alisema mtahiniwa huyo KCSE aliruka kutoka juu jengoni wasichana wengine walipokuwa wakijiandaa kwa shughuli za siku.
Naibu Kamishna wa Nyamira Kusini Florence Obunga alisema alifahamishwa kisa hicho na mwalimu mkuu mwendo wa saa kumi na mbili na nusu asubuhi.