Shangazi Akujibu

Sijawahi kuona miguu yake!

Na SHANGAZI November 18th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

SWALI: Kuna mwanamke ninayemtaka ingawa sijamwambia. Lakini ninashuku maumbile yake. Sijawahi kuona miguu yake kwani kila wakati huvaa nguo zinazoifunika. Nashuku anaficha kitu. Nishauri.

Jibu: Ni muhimu kupata mpenzi mwenye sifa unazopenda. Itabidi utafute namna ya kujua maumbile yake sehemu hiyo kabla hujamuomba penzi lake. Unaweza kutumia mmoja wa marafiki zake wa karibu akufanyie uchunguzi huo.

IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO