Wajiri yaagiza wafanyakazi warejee ofisini
Bruhan Makong
Kaunti ya Wajir imeagiza wafanyakazi wake warejee kazini baada ya miezi nne ya kukaa nyumbani. Hii ni baada ya usimamizi wa kaunti hiyo kuwaagiza wafanyakazi wake wasio wa muhimu sana wafanyie kazi nyumbani kwenye shughuli ya kupunguza kusambaa kwa virusi vya corona.
Tangu virusi vya corona viripotiwe Mwezi Mechi 13 Wajir imeripoti vusa 38 vya corona.Kitambo virusivya corona vilikuwa mingi lakini sasa vinaonekana kupungua.
Kwenye ujumbe alioutoa katibu wa kaunti hio Abdullahi Hassan Maalim alisema kwamba Kurudi kazini kutahakikisha huduma sahihi.
“Notisi hii inapeanwa ili kuwaita wafanyakazi wa kaunti kuruddi kazini ili waendelee kupeana huduma huku wakizingatia miongozo ya wizara ya afya.
Bw Maalim alisema pia virusi hivyo vya corona vitakaa sana kwa hivyo watu wanapaswa kujifunza kuishi navyo.
Wakuu wa Idara wanatakiwa kuhakikisha usafi wa maeneo ya kazi na na kuhakikisha kwamba wameweka vituo vya kuoshea mikono,kviyeyuzi,barakoa huku wafanyyakzi wakirudi kazini,”alisema.
Tafsiri na Faustine Ngila