Makala

LISHE: Wali na nyama iliyosagwa

November 9th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa mapishi: Dakika 30

Walaji: 4

Vinavyohitajika kwa wali

  • mchele kilo ½
  • tui la nazi kikombe 1
  • maji mara mbili kiasi ya mchele
  • chumvi
Wali. Picha/ Margaret Maina

Maelekezo

Osha mchele.

Weka mchele katika sufuria mekoni na ongeza chumvi. Acha mchele hadi uanze kuchemka.

Ukishaanza kuchemka, ongeza tui la nazi. Usikoroge.

Acha mchanganyiko uive taratibu kwa dakika 10.

Punguza moto na uache viive hadi maji yakauke.

Epua.

Vinavyohitajika kwa nyama ya kusaga

  • nyama ya kusaga kilo 1
  • vitunguu maji 2
  • vitunguu saumu 2
  • tangawizi 1
  • nyanya 4
  • mafuta ya kupikia
  • chumvi kijiko 1
  • pilipili mboga 1

Maelekezo

Menya vitunguu, pilipili mboga na ukate vipande vyembamba sana.

Menya nyanya na tangawizi kisha katakata.

Twanga vitunguu saumu kisha bandika sufuria ya kupikia mekoni.

Weka nyama na anza kukoroga isishikilie kwenye sufuria na kuungua.

Weka kitunguu maji huku ukiendelea kukoroga kwa muda wa dakika 10.

Ongeza kitunguu saumu na tangawiizi huku ukikoroga.

Weka mafuta ya kupikia kisha weka pilipili mboga. Ongeza chumvi kidogo. Endelea kukoroga.

Weka nyanya, koroga na funika sufuria halafu uache kwa dakika 10.

Pakua na wali wa nazi na ufurahie.