Kalameni akwepa ibada kusikia demu aliyemezea mate anapanga harusi na dume jingine kijijini
KIONGOZI wa vijana katika kanisa moja eneo la Bahati, Kaunti ya Nakuru, aliondoka kwenye ibada ghafla alipofahamu kuwa kidosho aliyekuwa mpenzi wake alikuwa akipanga harusi na polo mwingine.
Jamaa hakuweza kuvumilia kusikia tangazo la harusi la demu aliyemchukulia kuwa mpenzi wake wa dhati na mwanamume mwingine.
Aliondoka kwenye ibada na kuapa kutorudi kwenye kanisa hilo akisema hakuwa tayari kushuhudia kidosho aliyempenda akifunga pingu za maisha na jamaa mwingine.
“Siwezi kushuhudia mrembo niliyependa kwa dhati akienda na mwanaume mwingine,” polo alisema pasta alipomtembelea nyumbani kwake kujaribu kuelewa sababu yake ya kuhepa ibada.