Dondoo

Mama akaanga pasta kwa kuwapendelea waumini matajiri kanisani

Na DENNIS SINYO November 13th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

MAMA mmoja alishtua wenzake alipomtaka pasta wa kanisa lao amweleze sababu za kukataa kutembelea boma lake kwa mwaka mzima.

Mama huyo alidai amekuwa akituma barua kwa mchungaji huyo afike kwake kwa maombi ila maombi yake yamekuwa yakipuuzwa.

Alisema pasta alikuwa akitembelea waumini wengine katika maboma yao na akataka apewe sababu za kubaguliwa.

“Tunataka kujua iwapo kanisa hili ni la wadosi pekee yao au la. Mimi ni mmoja wa watu wa chini ambao tumebaguliwa sana na pasta. Nataka anieleze waziwazi ni kwa nini hataki kutembelea watu maskini,” aliwaka mama huyo.