Azuiliwa kwa kumuua rafikiye aliyemdai Sh500
Na Joseph Ndunda
Mkurugenzi wa kuendesha mashtaka wa DCI anazuilia mwendesha bodaboda aliyeua rafikiye aliyemdai Sh500.
Martin Mungai anayejulikana kama Sparta alimdunga kisu mwendazake kwa kukosa kumlipa deni .
Mshukiwa alikuwa mafichoni hadi Jumamosi iliyopita wakati alikamatwa kwa wizi wa bodaboda.
Bw Mungai aliachilia baada ya kutatua jambo hilo na mmiliki wa pikipiki lakini akakamatwa tena baada ya kugunduliwa kwamba alikuwa anatafutwa kwa kosa la mauaji.
Koplo Moses Kirima wa DCI Dandora alimuomba jaji mkuu Derrick Kuto kumruhusu aendelee kumuzuia Bw Mungai kwa siku 14 lakini lakini mshukiwa huyo alipinga hayo kupitia kwa wakili wake.
Bw Kuto aliruhusu Mungai aendelee kuzuiliwa na ajiwasilishe kortini Septemba 3.