Habari Mseto

Jaji ajiondoa katika kesi ya Martha Karua dhidi ya Gavana Anne Waiguru

February 13th, 2018 Kusoma ni dakika: 1

Kiongozi wa chama cha Narc Kenya Bi Martha Karua ambaye amewasilisha kesi kortini kupinga ushindi wa Gavana wa Kirinyaga Bi Anne Waiguru kwenye uchaguzi mkuu wa 2017. Picha/ Maktaba

Na RICHARD MUNGUTI

JAJI Otiendo Odek , wa Mahakama ya Rufaa Jumatatu alijiondoa katika kesi iliyowasilishwa na  kinara wa chama cha kisiasa cha Narc Bi Martha Karua.

Jaji Odek alijiondoa baada ya wakili Gitobu Imanyara kusema “Karua hana imani na uamuzi wa jaji huyo katika kesi ya kupinga kuchaguliwa kwa Gavana Ann Waiguru.”

Bw Imanyara alisema Jaji Odek atakuwa na upendeleo na hivyo basi akaomba ajiondoe.

Kufuatia madai hayo hilo Jaji Odek alijiondoa.

Mahakama Kuu ya  Kirinyaga ilitupilia mbali kesi ya kupinga ushindi wa Bi Waiguru.

Majaji Mohammed Warsame, Daniel Musinga na Odek walikuwa wameorodheshwa kusikiza rufaa hiyo.

Baada ya Jaji Odek kujiondoa, iliagizwa jaji mwingine ateuliwe na kesi kutengewa siku mpya ya kuisikizWa na kuamuliwa.