Uncategorized

Kisura ajuta kukataa mwalimu akidhani kalameni kutoka majuu atamuoa kumbe…

Na JANET KAVUNGA February 19th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

UAMUZI wa kipusa wa hapa wa kukataa mwalimu aliyemrushia mistari akimezea mate polo aliyerejea kutoka ng’ambo ulimponza jamaa huyo alipooa demu mwingine.

Kipusa alimkataa mwalimu huyo akidhani polo aliyetoka ughaibuni angemchangamkia kwa vile walikuwa wakiwasiliana mara kwa mara kwa kipindi cha miaka mitatu.

Hata hivyo, jamaa huyo alifunga harusi na mwanamke mwingine kutoka eneo la Kwale waliyekutana naye ng’ambo wanakofanya kazi. Iliibuka kuwa jamaa huyo alikuwa amerejea nchini kufanya harusi kisha yeye na mkewe warudi ughaibuni.

Demu alibaki kwa mataa na akatamani kufufua uhusiano wake na mwalimu ambaye tayari alikuwa amechumbia mwanadada mwingine na kwa sasa amebaki pweke.