Habari Mseto
Mbunge ashangaa kina mama kuchangamkia harusi kuliko elimu
NA WINNIE ATIENO
MBUNGE wa Changamwe, Bw Omar Mwinyi, amewakosoa baadhi ya wazazi Pwani, hasa kina mama, kwa kuthamini sana harusi badala ya masomo ya watoto wao.
Mbunge huyo alifedheheshwa na jinsi baadhi ya jamii za eneo hilo huwekeza pesa na muda mwingi kuandaa harusi kuliko jinsi wanavyofanyia elimu.
“Harusi ni muhimu lakini elimu ni muhimu zaidi,” alisema, akiwataka wazazi kudadisi namna wanavyolea watoto wao.