Habari Mseto

Najua nina jina kubwa, lakini mimi maskini hohehahe, mjukuu wa Moi aambia korti

Na JOSEPH OPENDA November 8th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

HUKU akikabiliwa na hatari ya kufungwa jela tena miezi miwili tu baada ya kutumikia kifungo cha wiki moja gerezani kwa kukiuka maagizo ya kuwatunza watoto wake, Collins Kibet, mjukuu wa marehemu Mzee Daniel arap Moi sasa anaiomba mahakama kutozingatia kuwa anatoka familia yenye jina kubwa.

Bw Kibet ambaye amepewa notisi kuonyesha kwa nini asiadhibiwe kwa kudharau mahakama, alikata rufaa mahakamani akitaka achukuliwe kama yatima maskini, bila kuzingatia familia kubwa tajiri anayotoka.

Bw Kibet anaitaka mahakama kumchukulia jinsi alivyo, bila kuzingatia jina la familia ya Moi, ambalo kulingana naye halijamsaidia kushinda changamoto za kimaisha.

“Ninaomba mahakama hii inichukulie kama Collins Kibet Toroitich na sio kwa mtazamo wa familia kubwa ya watu mashuhuri ninakotoka,”alisema Bw Kibet.

Akijibu kesi ya iliyowasilishwa dhidi yake na aliyekuwa mke wake Gladys Jeruto Tagi, Bw Kibet alidai kuwa maskini, ambaye anategemea usaidizi wa wasamaria wema na marafiki.

Inetafsiriwa na Benson Matheka