Wazee na akina mama wazua kizaazaa waking’ang’ania chapati kwenye sherehe
SINEMA ya bure ilishuhudiwa kwenye sherehe ya kulipa mahari eneo hili akina mama na wazee walipong’ang’ania chakula.
Inasemekana mambo yalikuwa shwari na walioalikwa walipata lishe ya kutosha lakini kizaazaa kilianza wakati wa kupatiwa chapati baadhi ya kina mama walipokosa subira na kufika kwenye meza ya wapishi wakitaka waongezewe chapati.
“Wengine walipata chapati mbili au tatu isipokuwa sisi. Tunawezaje kukosa ilhali mmejaza chapati kwenye ndoo?” mama mmoja alisema.
Hali ilipochacha, mpishi mmoja aliwapa ndoo ya chapati na kuwataka kujipanga wenyewe na wakaanza vurugu hadi ikawa vigumu kuwadhibiti kwani kila mmoja aling’ang’ana kuingiza mkono ndani ya ndoo.