Dimba

Man United yazinduka usingizini na kung’ata mtu hatimaye

Na MASHIRIKA November 4th, 2026 Kusoma ni dakika: 2

BAYERN Munich na Paris Saint-Germain (PSG) zimeimarisha matumaini yao ya kutwaa taji la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) baada ya kupata ushindi mnono dhidi ya Atletico Madrid na Villarreal mtawalia Jumanne usiku.

Manchester United ilionyesha juhudi za kupambana kwa kurejea kutoka nyuma kwa mabao mawili na kuichapa AS Roma 3-2 katika mechi ya kusisimua kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Bayern ilipata ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya Atletico Madrid, ambayo iliwasumbua kwa muda mrefu.

Lennart Karl aliifungulia Bayern ukurasa wa mabao dakika ya 54 kabla ya Konrad Laimer kuongeza la pili dakika ya 74, akitumia pasi ya Harry Kane.

PSG nayo iliweka rekodi kwa kufunga mabao manne ndani ya dakika 17 za mwanzo katika ushindi wa 6-0 dhidi ya Villarreal.

João Neves, Désiré Doué na Senny Mayulu walifunga mabao matatu ndani ya kipindi cha dakika tano kabla ya Fabián Ruiz kuongeza la nne.

Ruiz alifunga tena kipindi cha pili kabla ya David Boly, aliyekuwa akicheza mechi yake ya kwanza katika mashindano hayo, kukamilisha karamu ya mabao.

Katika Uwanja wa Old Trafford, Manchester United ilijipata nyuma kwa mabao mawili baada ya Matías Soulé na Donyell Malen kuifungia Roma. Malen alifunga kupitia penalti.

Hata hivyo, Bruno Fernandes aliipatia United bao la kwanza kupitia penalti iliyopigwa upya kabla ya Matheus Cunha kufunga mabao mawili ndani ya dakika nne na kuipa timu hiyo ushindi wa 3-2.

Barcelona nayo iliilaza Aston Villa 3-0. Lamine Yamal alifungua ukurasa wa mabao dakika ya saba kabla ya Raphinha kufunga mawili kipindi cha pili, akitumia nafasi iliyotokana na shuti iliyopanguliwa na baadaye pasi ya João Cancelo.

Inter Milan iliicharaza Feyenoord 3-0. Yann Bisseck alifungua ukurasa wa mabao kwa shuti ya mbali kabla ya Pio Esposito kuongeza la pili kwa kichwa kutokana na krosi ya Djed Spence. Piotr Zielinski alikamilisha ushindi huo kwa shuti kali ya mbali kipindi cha pili.

Katika mechi nyingine, Galatasaray iliilaza Stuttgart 2-0 kupitia mabao mawili ya Aleksei Batrakov. Sporting CP iliishinda Shakhtar Donetsk 1-0 kupitia Issa Doumbia.

LASK nayo iliichapa Slovan Bratislava 4-0 ambapo Kasper Jørgensen alifunga mawili, Robert Ljubičić akaongeza la tatu na Samuel Adeniran akafunga la nne. Bodø/Glimt na Lille zilitoka sare ya 0-0.

PSG inaongoza msimamo kwa alama 12, huku Barcelona na Aston Villa zikiwa miongoni mwa timu sita zilizo na pointi tisa.

Kabla ya mechi hizo, viwanja mbalimbali barani Ulaya vilikaa kimya kwa dakika moja kuomboleza kifo cha mchezaji wa Tenerife, Jesus de Miguel, aliyefariki dunia Jumanne.

Ratiba ya Europa League:

Milan v Ferencavaros (20.45pm)

Palace v Hoffenheim (20.45pm)

Sparta Braha v Bournemouth (20.45pm)

NEC v Omonio (20.45pm)

Anderlecht v RB Salzburg (20.45pm)

Real Sociedad v OL (20.45pm)

Levski Sofia v Jagiellonia (20.45pm)

Torreen v Ararat-Armenia (23.00pm)

Celtic v Besikitas (23.00pm)

Sturm Graz v Celjie (23.00pm)

H-Beersh-Sheva v OFI (23.00pm)

AZ v Juventus (23.00pm)

Leverkusen v Marsaille (23.00pm)

Benfica v Lech Poznari (23.00pm)