Habari Mseto

Mawakili wataka korti zifunguliwe mrundiko wa kesi upungue

March 30th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

PHILIP MUYANGA NA FAUSTINE NGILA
Wito  kwa Jaji Mkuu David Maraga kubatilisha uamuzi wake wa kufunga mahakama kote nchini umepata shinikizo mpya Jumatatu. 

Chama cha Mawakili tawi la Mombasa kimesema kuwa katiba haiwezi kutekelezwa katika hali ambayo korti zimefungwa.

Mwenyekiti wa chama hicho Mathew Nyabena alisema kuwa Jaji Mkuu anapaswa kubadilisha uamuzi wake na kuruhusu shughuli za kawaida kuendelea kila siku kwa kufuatilia hali ya  janga la corona.

“Tunawaomba baadhi ya mahakimu wawe wakishughulikia maswala ya kila siku,” alisema Bw Nyabena, akiongezea kuwa kunapaswa kuwa na wafanyakazi wachache katika afisi za usajili kushungulikia  kukusanya stakabathi za mawakili na washtakiwa.

Bw Nyabena aliogezea kuwa kuna kesi za dharura ambazo zinapaswa kusikizwa kwa wakati unaofaa.

Alisema kuwa Jaji Mkuu amezuia  majaji na wakuu wa vituo kubuni mbinu mbadala za kufanya kazi,

Bw Nyabena alisema kuwa imekuwa kazi ngumu kwa mawakili kutekeleza majukumu yao kutokana na notisi iliyotolewa kuwa  ni kesi za dharura pekee zitakazosikizwa kila Alhamisi pekee.