LISHE: Keki ya vanilla isiyo na mayai
NA WANGU KANURI
Jinsi ya kuandaa keki
Muda wa kuandaa: dakika kumi
Muda wa kuoka: dakika thelathini
Viungo
- Vikombe vitatu vya unga wa ngano
- Kikombe kimoja cha sukari
- Kijiko nusu cha chai cha chumvi
- Kikombe kimoja cha mafuta ya kupika
- Viikombe viwili vya maziwa iliyoganda ama maziwa kawaida
- Vijiko viwili vya kulia vya unga wa kuoka
- Vijiko vinne vya chai vya vanilla
- Kikombe kimoja cha sukari laini (icing sugar)
- Kijiko kimoja cha chai cha maziwa
- Chakuleti iliyoyeyuka
Maelekezo
- Pasha tanuri yako kwa moto wa nyuzi 170.
- Changanya unga, sukari, na chumvi pamoja. Hakikisha umechanganya vizuri.
- Ongeza viowevu kwenye mchanganyiko wako. Viowevu hivyo ni mafuta ya kupika, maziwa
- yaliyoganda na vanilla. Hakikisha umechanganya vizuri lakini sio sana. Mtiririko usiwe laini
- sana.
- Paka majarini kwenye bakuli ya kuokea kisha umimine mchanganyiko huo kwenye bakuli hiyo.
- Oka kwa muda wa dakika thelathini.
- Baada ya keki kupoa, changanya kikombe kimoja cha sukari laini na kijiko kimoja cha maziwa
- kisha mwaga kwenye keki.
- Unaweza kuongeza chakuleti iliyoyeuka kwenye keki yako.