Coca-Cola yatoa Sh42 milioni kushindaniwa na Wakenya wakisubiri Kombe la Dunia
Na CHRIS ADUNGO
KAMPUNI ya vinywaji ya Coca-Cola itawatuza watumiaji wa bidhaa zake milioni mbili, mwaka huu katika kipute cha Kombe la Dunia unaopangiwa kuanza mwezi Juni nchini Urusi.
Katika kampeni yake ya Funga Mamili na Coca-Cola, watakaotumia bidhaa zao kwa wiki kumi na sita zijazo watakuwa na nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali za thamani ya Sh42.5 milioni.
“Coca-cola imekuwa mdhamini wa Kombe la Dunia kwa zaidi ya miongo minne sasa. Katika matayarisho ya kombel hili la FIFA, tunalenga kutumia msisimko wa Wakenya wanaopenda soka na kuwazawadi kupitia kampeni hii.
Zawadi hizo zinawapa nafasi mbalimbali za kujitayarishia mchezo huo kwa kuwafanya watu millionia kumi na sita mamilionea mwishoni mwa kampeni hio,” akasema Rodney Nzioka mwadamizi, meneja wa brandi ya kampuni hiyo.
Bidhaa zitakazotumiwa katika ukuzaji huu ni pamoja na soda za Coca-cola, Sprite, Krest na Stoney zitakazokuwa kwa chupa za plasitiki ama kioo ambazo zitakuwa na kifuniko cheupe zitakazopatikana madukani kote nchini.
Pesa taslimu za kushindaniwa ni kati ya shilingi mia tano na milioni moja, zawadi zinginezo zikiwa runinga za dijitali, vifushi vya data, na malipo ya runinga.
Watakaoshiriki lazima wawe wamajisajili kama watumiaji wa huduma za simu za mkononi za mitandao ya Safaricom, Airtel,
Kushiriki unahitajika kutuma nambari nane kwenye kifuniko kwa nambari 40111 ili kupata nafasi ya kujishindia zawadi kila siku na kila wiki.