PATA USHAURI: Fahamu ugonjwa wa homa ya ini
Na PAULINE ONGAJI
HOMA ya ini au Hepatitis B ni ugonjwa wa kuambukizwa unaotokana na virusi vya Hepatitis B Virus (HBV).
Japo maambukizi haya ni hatari sana na yaweza kusababisha kifo endapo hayatatibiwa, yaweza kuzuiwa kwa kutumia chanjo.
Unavyoambukizwa
• Kujamiana bila kinga
• Kupigana denda
• Kuchangia damu isiyo salama
• Kuchangia sindano, wembe, miswaki, au hata taulo
• Mama mwenye ugonjwa kumwambukiza mtoto wakati wa kujifungua
Lazima mgonjwa akaguliwe na mtaalamu wa kimatibabu ambapo mara nyingi uchunguzi kwenye maabara huhitajika.
Ishara
• Uchovu na mwili kuwa dhaifu
• Kichefuchefu
• Homa kali
• Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito.
• Maumivu makali ya tumbo upande wa ini
• Macho na ngozi kuwa manjano
• Mkojo mweusi au wa utusiutusi
Kwa waathiriwa wengi, hali huwa mbaya zaidi na kusababisha saratani ya ini.
Kinga
• Chanjo
• Kutumia kinga wakati wa kujamiiana
• Kuacha kuchangia sindano, wembe, miswaki au hata taulo
Unashauriwa kutumia vyakula vinavyosaidia kuua bakteria na virusi hasa vyenye kuongeza kinga mwilini kama vile matunda na mboga.