Dondoo

Mpango wa kando anyima buda usingizi alipotishia kumuachia mtoto afisini kwake

Na JANET KAVUNGA January 28th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

BUDA mmoja wa hapa alilazimika kumuacha mkewe usiku kwenda kumtuliza mpango wake wa kando aliyetishia kumpelekea mtoto aliyemzalisha ofisini.

Buda alikuwa amehepa demu tangu ajifungue na hata akaacha kumtumia pesa za mahitaji.

Mwanadada alimtumia ujumbe usiku akimwambia kuwa atampata  mtoto katika ofisi yake asubuhi kwa kuwa alikuwa amempuuza kwa muda mrefu.

Jamaa alipopata ujumbe huo alikosa usingizi akamweleza mkewe kuwa alikuwa amepata dharura kisha akaelekea kwa demu kumtuliza.

Kulingana na demu, buda aliahidi kumtimizia mahitaji yote na ya mtoto ili asimuabishe.

“Aliniomba nisimuaibishe akisema hakuwa amehepa majukumu yake kama baba mtoto,” demu alisimulia marafiki katika ukurasa wa mademu kupashana masaibu yao ya mahusiano.