Mcheza kamari taabani kwa kuwatusi polisi
Na RICHARD MUNGUTI
MCHEZAJI Kamari aliyeenda kutafuta riziki katika Jokers Casino jijini Nairobi alishtakiwa kwa kuwatusi maafisa wa polisi.
Bw Kennedy Okoth Aete alifikishwa mbele ya hakimu mwandamizi Kennedy Cheruiyot, Milimani.
Alikanusha mashtaka mawili dhidi yake.
Alikabiliwa na shtaka la kuzua vurugu kwa lengo la kuhatarisha amani kwa kuwatusi maafisa wa polisi – maneno ambayo hayawezi kuchapishwa.
Bw Aete aliomba aachiliwe kwa dhamana isiyo ya kiwango cha juu.
Aliachiliwa kwa dhamana ya Sh20,000.