• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 8:50 AM
Musiala atia saini kandarasi ya kuchezea Bayern hadi 2026

Musiala atia saini kandarasi ya kuchezea Bayern hadi 2026

Na MASHIRIKA

FOWADI Jamal Musiala, 18, ametia saini mkataba wake wa kwanza wa kitaaluma na kikosi cha Bayern Munich nchini Ujerumani.

Hatua ya chipukizi huyo inafanyika wiki chache baada ya kuteua kuchezea Ujerumani badala ya Nigeria au Uingereza katika soka ya kiwango cha kimataifa.

Musiala alipokezwa malezi ya soka katika akademia ya Chelsea kabla ya kuingia katika sajili rasmi ya Bayern mnamo 2019.

Sogora huyo ametia saini kandarasi ya kwanza rasmi katika kikosi cha Bayern hadi 2026. Kufikia sasa, amefungia miamba hao wa soka ya Ujerumani, bara Ulaya na dunia jumla ya mabao manne kutokana na mechi 27.

Mnamo Februari 2021, Musiala aliweka historia ya kuwa mwanasoka mchanga zaidi kuwahi kufunga bao katika soka ya UEFA. Alikuwa miongoni mwa wafumaji wa magoli katika ushindi wa 4-1 uliosajiliwa na Bayern dhidi ya Lazio kwenye mkondo wa kwanza wa hatua ya 16-bora ya UEFA nchini Italia.

Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Loew amethibitisha kwamba Musiala atakuwa sehemu ya kikosi kitakachotegemewa na mabingwa hao wa zamani wa dunia katika mechi zijazo za kimataifa mwezi huu wa Machi 2021.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Lewandowski aongoza Bayern kuzamisha Dortmund

Mwatate yajiandaa kuonyesha ubabe wake Kisumu Jumatatu