• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 9:50 AM
Mvamizi kigogo Andy Carroll avunja ndoa na Newcastle United kwa mara ya pili

Mvamizi kigogo Andy Carroll avunja ndoa na Newcastle United kwa mara ya pili

Na MASHIRIKA

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

MSHAMBULIAJI wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, Andy Carroll, 32, sasa anatafuta klabu mpya ya kumpa hifadhi baada ya kuagana na Newcastle United.

Carroll alijiunga upya na Newcastle mnamo 2019 kutoka West Ham, miaka minane baada ya kubanduka uwanjani St James’ Park na kuyoyomea Liverpool kwa Sh5.4 bilioni.Hata hivyo, alitatizwa pakubwa na majeraha huku akiwajibishwa na kocha Steve Bruce wa Newcastle mara nane pekee katika mechi za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo 2020-21.

Nyota huyo alichezea Uingereza mara tisa kati ya 2010 na 2012 ambapo alipachika wavuni mabao mawili – dhidi ya Ghana kirafiki na dhidi ya Uswidi kwenye kipute cha Euro 2012.

Kwa mujibu wa Bruce, kuondoka kwa Carroll ambaye mkataba wake ulikatika rasmi mnamo Juni 30, kutawapa vinara wa Newcastle msukumo zaidi wa kumsajili chipukizi Joe Willock wa Arsenal aliyewachezea kwa mkopo muhula uliopita.

Willock, 21, alifungia Newcastle mabao manane katika mechi 14 na kusaidia kikosi hicho kukwepa shoka ambalo vinginevyo, lingekishuka ngazi kwenye EPL. Newcastle walikamilisha kampeni za EPL 2020-21 katika nafasi ya 12 jedwalini kwa alama 45 sawa na Wolves ambao sasa wanatiwa makali na kocha Bruno Lage aliyechukua mahali pa Nuno Espirito aliyeajiriwa na Tottenham Hotspur.

  • Tags

You can share this post!

Atlanta yamtimua kocha Gabriel Heinze baada ya kusimamia...

Rashford kukaa nje kwa miezi miwili akiamua kufanyiwa...