• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 5:55 AM
Kocha Nuno Espirito wa Wolves atozwa faini ya Sh3.5 milioni kwa utovu wa nidhamu

Kocha Nuno Espirito wa Wolves atozwa faini ya Sh3.5 milioni kwa utovu wa nidhamu

Na MASHIRIKA

MKUFUNZI Nuno Espirito Santo wa Wolves ametozwa faini ya Sh3.5 milioni na Shirikisho la Soka la Uingereza (FA) kwa kumchemkia na kumkosoa refa Lee Mason wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) iliyowakutanisha na Burnley uwanjani Turf Moor mnamo Disemba 21, 2020.

Burnley waliibuka washindi wa mechi hiyo kwa mabao 2-1. Mwishoni mwa mechi hiyo, Nuno alisema kwamba refa Mason “hakumakinikia majukumu yake na hastahili kuwa mwamuzi wa mechi za haiba kubwa kwa sababu alionekana kama ambaye hajahitimu kwa kazi yake.”

Nuno baadaye alikataa kuomba radhi kutokana na matamshi yake japo alikiri kwamba yalidhihirisha kiwango fulani cha utovu wa nidhamu kwa upande wake.

Mbali na kutozwa faini, FA imemwonya vikali kocha huyo raia wa Ureno na kumtaka arekebishe mienendo yake katika ulingo wa soka.

Nuno aliitaka madai dhidi yake yachunguzwe na jopo huru la nidhamu lililobaini kwamba matamshi yake kumhusu Mason yalikuwa ya kiuchochezi na ya utovu wa nidhamu kiasi cha kupaka tope ubora wa viwango vya soka ya EPL ambayo ni mojawapo ya mashindano makuu ya haiba kubwa barani Ulaya.

Kwa mujibu wa kanuni za FA, kauli za wanasoka na makocha kuhusu wasimamizi wa mechi baada ya mchuano zinakubaliwa tu kukosoa matokeo ya uwanjani wala si kujikita katika masuala ya mapendeleo, uadilifu wa refa au utendakazi wake.

  • Tags

You can share this post!

COVID-19: Kenya yathibitisha visa vipya 271 idadi jumla...

KNPC yataja kikosi cha Riadha za Walemavu za Dubai Para...