• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 5:55 AM
Onyo magaidi wasajili watoto mitandaoni

Onyo magaidi wasajili watoto mitandaoni

Na MARY WAMBUI

WAZAZI wametakiwa wafuatilie mienendo ya watoto wao ili kuwazuia kujiunga na makundi ya kigaidi kupitia ueneaji wa itikadi kali hasa kupitia mitandaoni wakati huu ambapo shule zimefungwa na wako likizoni.

Kituo cha Kitaifa cha Kupambana na Ugaidi (NCTC) kinasema kwa sasa makundi ya uhalifu yanaendeleza tabia zao kupitia ulanguzi wa mihadarati. Kituo hicho kimeonya kuwa kutakuwa na ongezeko la matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa wanafunzi wengi shuleni kupitia ripoti ya Shirika la Kupambana na Matumizi ya Mihadarati (NACADA) 2019.

Ripoti hiyo ilifichua kuwa watoto wadogo kuanzia umri wa miaka minne wamezamia matumizi ya dawa za kulevya. Hii ni kwa sababu matumizi ya dawa hizo sasa yamekithiri shuleni hasa unywaji pombe.

Wengi wa wanafunzi wanaozamia matumizi ya dawa za kulevya hufanya hivyo kutokana na msukumo wa kuwaiga wenzao pamoja na kutimiza mahitaji ya kibinafsi iwapo wanatoka katika familia maskini.

“Imebainika kuwa ni rahisi mno kwa watoto wanaotumia dawa za kulevya kujiunga na makundi ya uhalifu na yale ya kigaidi. Wao hufanya hivyo ili waendelee kupata dawa hizo kwa kuwa uraibu wa kuzitumia ushawaingia,” ikasema ripoti ya NCTS kuhusu usalama wa watoto na katika uzuiaji wa wanafunzi wa shule mbalimbali kukumbatia uhalifu na ugaidi.

Aidha, wazazi wameshauriwa kutazama dalili kadhaa kuonyesha mtoto amejiunga na makundi haya ya uhalifu. Moja ni matumizi ya mara kwa mara ya mitandao ya kijamii ambapo wao huandika mambo yasiyotaka maoni ya wengine. Hasa masuala wanayojihusisha nayo huwa ni ya kueneza ghasia.

Dalili nyingine ni mtoto kujitenga na kuwa pekee yake mara nyingi huku akikasirikia mambo madogo madogo na kujisawiri kama asiyeridhika maishani.

Pia yeye hubadili mtindo wake wa mavazi hasa kupendelea nguo zinazofanana na za polisi na kukumbatia mtindo wa kiajabu wa kutengeneza nywele.

Mkurugenzi wa NCTS Joseph Opondo alisema kwamba wazazi ndio wanajukumu kubwa la kuwazuia wanao kujiunga na makundi ya ugaidi au magenge ya wezi hasa enzi hizi za utandawazi ambapo wanaweza kufikia mambo mengi kwa urahisi.

You can share this post!

Leicester waaibisha Manchester United na kufuzu kwa...

Wanaume makahaba waongezeka Mombasa