• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 11:46 AM
Jina la Martha Koome latua bungeni

Jina la Martha Koome latua bungeni

NA CHARLES WASONGA

Rais Uhuru Kenyatta Jumatano amewasilisha jina la Jaji Mkuu mteule Martha Koome katika Bunge la Kitaifa.

Spika Justin Muturi amesoma ujumbe kutoka kwa Rais akiomba bunge hilo limpige msasa Jaji Koome kubaini ufaafu wake kwa wadhifa huo.

Spika ameamuru Kamati ya Bunge kuhusu Haki na Masuala ya Sheria (JLAC) kuandaa vikao vya kumdadisi Jaji Koome kisha iwasilishe ripoti yake kwa kikao cha bunge lote baada ya siku 28.

Hii ina maana kuwa kamati hiyo inayoongozwa na mbunge wa Kangema Muturi Kigano itawasilisha ripoti yake mnamo 25/5/ 2021.

Hata hivyo, kwa kuzingatia dharura iliyoko kamati hiyo imetakiwa kuandaa ripoti yake “haraka iwezekanavyo”

You can share this post!

Wawili wanaswa na noti feki za Sh750 milioni

Serikali yazima Mt Kenya TV kwa kupotosha watoto