• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
Mahabusu alalama Kortini hakupewa chakula akiwa rumande

Mahabusu alalama Kortini hakupewa chakula akiwa rumande

Na RICHARD MUNGUTI

RAIA wa Kenya aliyeshtakiwa kwa kughushi cheti cha kusafiri kutoka Afrika kusini kuhepa ghasia na vurugu iliyotokea kufuatia kusukumwa jela kwa aliyekuwa Rais Jacob Nzuma alidai mahakamani alinyimwa chakula alipozuiliwa katika kituo cha polisi cha Capital Hill Nairobi.

Bw Bishar Maulid Hassan aliyeshtakiwa mbele ya hakimu mkuu mahakama ya Milimani Bw Francis Andayi alisema “hakukuwa na chakula cha kutosha katika kituo cha polisi cha Capital Hill nilipozuiliwa.”Akasema Bw Hassan,” Mheshimiwa sijakula tangu nilipozuiliwa katika kituo cha Polisi cha Capital.”

Bw Andayi alimwuliza, “Unamaanisha tangu ulipozuiliwa hukupewa chakula hata kidogo.”Mshtakiwa alijibu alipewa tu Ugali na Kebeji.Hakimu alimuhoji zaidi, “ Je ulipata kifungua kinywa asubuhi kabla ya kuletwa mahakamani?”

Alijibu , “ Nilipewa tu Chai na Andazi na sikushiba.”Bw Andayi alimjibu na kumweleza ashukuru kwa chakula alichopewa.Bw Hassan alikabiliwa na shtaka la kupatikana na cheti cha usafiri cha Serikali ya Afrika kusini alichokighushi.

Shtaka lilikuwa alipatikana na cheti hicho mnamo Agosti 7 2021 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JomoKenyatta.Mshtakiwa huyo alieleza mahakama kule Afrika kusini mmoja akizuiliwa rumande anapewa chakula cha kutosha na godoro.

“Kule Afrika kusini washukiwa hupewa chakula cha kutosha na godoro la kulalia sio kama hapa mahabusu hulala kwa sakafu,”alisema Bw Hassan.Mshtakiwa alidaiwa cheti alichokuwa nacho kilikuwa kimetolewa na Afisa mwandamizi wa Idara ya Uhamiaji wa Afrika kusini.

Hakimu aliamuru afisa wa urekebishaji tabia ahoji watu wa familia ya mshtakiwa kabla ya kumwachilia na dhamana.

  • Tags

You can share this post!

Haji aamuru polisi sita washtakiwe kwa mauaji ya ndugu...

AFYA: Umuhimu wa mazoezi kwa wajawazito