• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 12:11 PM
Serikali yafunga shule yenye madarasa hatari Mukuru

Serikali yafunga shule yenye madarasa hatari Mukuru

Na SAMMY KIMATU

SHULE moja miongoni mwa nyingine tatu za wamiliki binafsi zilizofungwa katika maeneo ya Mukuru, Kaunti ya Nairobi kwa kutofuata maagizo ya Wizara ya Elimu ni rasmi haitafunguliwa tena.

Shule ya Joyland Children Centre ilioko katika mtaa wa Mukuru-Hazina, Tarafa ya South B kwenye kaunti ndogo ya Starehe haitafunguliwa milango yake tena. Akiongea na wanahabari jana, chifu wa Lokesheni ya Mukuru-Nyayo, Bw Charles Mwatha alisema majengo ya shule ya Joyland yalikuwa hatari kwa usalama wa watoto. ’’Serikali iliifunga rasmi kwani madarasa yake yalihatarisha usalama wa watoto. Kando na hayo, aliyekodi shule hiyo alikuwa na malimbikizo ya deni ya shule kati yake na mwenye ploti pesa zilizodaiwa kuwa zaidi ya Sh200,000,’’ chifu Mwatha akasema. Aidha, aliongeza kwamba wanafunzi walihamishwa hadi shule zingine katika eneo la South B.

Watahiniwa wa Darasa la Nane waliliosajiliwa mwaka 2020 watafanyia mtihani wa KCPE katika Shule ya Baptist Academy.

Katika lokesheni hiyo pia, Shule ya The Rock Academy iliyogeuzwa kuwa nyumba za kukodishwa kufuatia shule kufungwa kote nchini baada ya janga la corona imegeuzwa kuwa shule tena.

“Niliamua kukodisha watu yaliyokuwa madarasa ambayo niliyageuza vyumba vya kulala ili nipate pesa za kujikimu muda huo shule zilifungwa kwa miezi karibu kumi,’’ Bi Christine Kathukya, Mkurugenzi wa The Rock Academy akasema.

Jana Jumanne, walimu na wanafunzi walikuwa darasani wakisoma kama ilivyokuwa ada. Hatua chache kutoka kwa shule hiyo, shule nyingine ya kibinafsi ilihamia kusikojulikana. Shule ya Ridgeville Academy ilihama kutoka mtaa wa Hazina na badala yake jana nafasi yake ilichukuliwa na shule nyingine ya kibinafsi kutoka kaunti ndogo ya Kibera

You can share this post!

Visa 40 vya maambukizi ya Covid-19 vyaripotiwa miongoni mwa...

ULIMBWENDE: Ndizi na urembo