• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
Washukiwa watatu wa uhalifu wa kiteknolojia wanaswa Juja

Washukiwa watatu wa uhalifu wa kiteknolojia wanaswa Juja

Na LAWRENCE ONGARO

WASHUKIWA watatu wa uhalifu wa kiteknolojia wamenaswa eneo la Juja, Kaunti ya Kiambu.

Washukiwa hao walinaswa Ijumaa jioni katika nyumba moja wakiendesha shughuli zisizo sawa.

Afisa wa upelelezi wa Juja Bw Richard Mwaura, alisema watu hao walipatikana na kadi 100 zilizosajiliwa za kampuni ya Safaricom.

Wakati huo huo, pia wanaume hao walipatikana na vitambulisho kadha vya watu huku ikishukiwa walikuwa na njama fulani fiche.

Wakati huo pia ilidaiwa washukiwa hao walipatikana na bangi misokoto 20 ambapo wanaume hao walikuwa wa umri wa kati ya miaka 22 na 25.

“Tunashukuru wananchi kwa kuwa mstari wa mbele kuarifu polisi kuhusu vitendo vya washukiwa hao,” alisema afisa huyo wa upelelezi.

Alieleza kuwa washukiwa hao watahojiwa na kitengo cha Multi Agency Team na kile cha Cybercrime ili kubaisha ukweli wa mambo.

Alisema baada ya uchunguzi kamili kukamilika ndipo watafunguliwa mashtaka kuhusu ulaghai kwenye mitandao na simu.

Afisa huyo alipongeza wananchi kwa kushirikiana na polisi kwa kufanikisha kunaswa kwa washukiwa hao.

“Tungetaka wananchi wawe na msimamo huo ili wale wanaokuwa na mambo maovu wanaswe mapema,” alisema afisa huyo wa upelelezi.

Alisema wanashuku pia ni watu wengi ambao vitambulisho vyao vinatumika bila wao kujua.

Safaricom inahitajika pia kupeleleza zaidi kung’amua ukweli wa mambo.

  • Tags

You can share this post!

Biden ataka bunge kukinga wanaoshindwa kulipa kodi

Uhispania wakomoa Ivory Coast na kufuzu kwa nusu-fainali za...