• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 12:56 PM
Polisi aua 7 akiwemo mkewe kabla kujiua

Polisi aua 7 akiwemo mkewe kabla kujiua

DANIEL OGETA, MARY WANGARI na BENSON MATHEKA

SERIKALI imesukuma maafisa wa polisi kuzama katika mfadhaiko na mzongo wa mawazo na kusababisha ukatili kama ulioshuhudiwa jana ambapo afisa mmoja aliwaua watu saba, akiwemo mkewe kabla ya kujiua.

Konstebo Benjamin Imbasi alimuua mkewe na watu wengine sita kwa kuwapiga risasi, kabla ya kujitoa uhai katika kisa cha kushtusha usiku wa manane mjini Kabete, Kaunti ya Kiambu.Wanasaikolojia wanasema maisha magumu, kunyanyaswa na wakubwa, presha ya kazi na hali ngumu ya kiuchumi ni miongoni mwa changamoto zinazosukuma maafisa wa polisi kuzama katika mfadhaiko na kutenda ukatili.

Kikosi cha polisi hufanya kazi na kuishi katika mazingira magumu yenye shinikizo tele, yanayowasababishia matatizo ya kisaikolojia, kifamilia na kijamii.Mwanasaikolojia Paul Ngunyi, mwanzilishi wa Better People Academy anasema kuwa, licha ya kuwa maafisa wa polisi wanahitaji msaada zaidi kutokana na shinikizo za taaluma yao, serikali na wadau husika hawajitahidi vya kutosha kuboresha maslahi ya kikosi cha walinda usalama nchini.

“Kazi ya polisi ni tofauti na ina presha nyingi ikilinganishwa na taaluma zingine. Kutokana na shinikizo za kikazi, baadhi ya maafisa wa polisi huwa hawana muda kabisa na familia zao, hasa ikizingatiwa huwa wanahamishwa mara kwa mara.

Matarajio ya kifamilia kwa mfano kati ya mume na mke huwa hayatimizwi hivyo kusababisha mafarakano katika ndoa. Wengi wao huishia kupeleka masaibu yao ya kikazi nyumbani,” akasema Bw Ngunyi.Na jana, Waziri wa Usalama wa Ndani, Fred Matiang’i alisema kisa cha polisi aliyeua watu saba Kabete kinachunguzwa na kwamba, serikali inashughulikia afya ya akili ya maafisa wa polisi.

Alikiri maafisa wa polisi wanakabiliwa na matatizo ya akili laikini akawaonya walioeneza uvumi kuhusu kisa hicho na vingine vya matatizo ya akili ya maafisa wa polisi akisema wanaathirika kama watu wengine.“Kilichotendeka kinahuzunisha lakini tuwajibike.

Ni suala linaloathiri jamiii na kila mmoja anafaa kuwajibika badala ya kulaumu maafisa wa polisi,” alisemaKatika mkasa wa jana, Bw Imbasi aliyejihami kwa bunduki aina ya AK 47 alimuua mkewe Carol katika nyumba za J Apartments kabla ya kutoka nje na kuwafyatulia risasi watu wengine, wakiwemo wanabodaboda wawili.

Kisa hicho kilifanya wakazi kuandamana huku wakifunga sehemu ya barabara ya Waiyaki kulalamikia ukatili wa askari huyo.Mkuu wa polisi kaunti ndogo ya Kabete, Francis Wahome alisema kwamba, haikujulikana kilichofanya afisa huyo kutekeleza ukatili huo.

Anasema serikali inafaa kuwachukulia maafisa wa usalama kama binadamu badala ya kuwatumia na kukosa kujali maslahi yao.Katika siku za hivi majuzi, Kenya imegubikwa na visa vingi vya maafisa wa polisi kuwageukia wapendwa wao na umma kwa jumla na kuwaua kikatili kabla ya kujitia kitanzi.

Mnamo Oktoba, afisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Masalani, Kaunti ya Garissa, alimuua mpenzi wake kwa kumdunga kisu kabla ya kujilipua. Katika kisa kilichotikisa nchi Agosti, Konstebo wa Polisi Bernard Sivo alimuua mkewe kwa kumpiga risasi mara 15 akiwa hospitalini kabla ya kujitoa uhai, eneo la Kwanza, Njoro.

 

You can share this post!

Ethiopia yatangaza hatua dhidi ya TPLF

Mzozo wa mpaka eneo la Maseno walipuka upya

T L