• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 5:50 AM
Ripoti ya utafiti yachora taswira ya viwango vya umaskini Afrika Kusini

Ripoti ya utafiti yachora taswira ya viwango vya umaskini Afrika Kusini

Na MASHIRIKA

PRETORIA, Afrika Kusini

KIWANGO cha ukosefu wa ajira nchini Afrika Kusini kimepanda hadi kuwa cha juu zaidi duniani, kulingana na utafiti wa hivi punde uliofanywa baina ya mataifa 82.

Kulingana na ripoti ya utafiti iliyoendeshwa na Shirika la Takwimu nchini humo, Statistic South Africa, ni mtu mmoja pekee kati ya watu wanne ndiye ameajiriwa.

Shirika hilo linaeleza, kwenye ripoti iliyotolewa Jumanne jijini Pretoria kuwa mlipuko wa janga la Covid-19 ulipandisha kiwango cha ukosefu wa ajira kutoka kiwango cha asilimia 32.2 hadi asilimia 34.4.

Idadi ya wale ambao wamesitisha juhudi za kusaka ajira nayo imepanda kwa kiwango cha asilimia 10 a kutoka asilimia 34.4 hadi asilimia 44.4.

Kulingana na wataalamu wa masuala ya kiuchumi, Afrika Kusini pia inakabiliwa na hali ya kiuchumi.

Wanasema janga la corona limezidisha hali mbaya ambayo ilichangiwa na utawala mbaya wa rais wa zamani Jacob Zuma.

Kiongozi huyo wa zamani sasa anatumikia kifungo cha miezi 15 gerezani kwa kukaidi amri ya kutakiwa kufika mahakama kujibu mashtaka ya ufisadi.

Tafsiri: CHARLES WASONGA

You can share this post!

KAMAU: Viongozi sasa waelekeze macho kwa umoja wa taifa

USWAHILINI: Huu hapa mseto wa milo inayopendwa mno katika...