• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 7:50 AM
Utawala bora wa chama cha CPC ni mfano wa kuigwa na Afrika

Utawala bora wa chama cha CPC ni mfano wa kuigwa na Afrika

NA MASHIRIKA

Kulingana na takwimu za benki ya dunia, mwaka 1960 China ilikuwa maskini kuliko baadhi ya nchi barani Afrika. Kwa mfano mwaka 1960, mgao wa pato la kitaifa kwa China ulikuwa dola 89 tu, wakati DR Congo ulikuwa dola 220, Kenya dola 97, Afrika Kusini 433 na Ghana 183.

Lakini ifikapo mwaka 2017 mgao huo kwa China ulikuwa umefikia dola 8,827, huku Kenya ikiwa na dola 1,507, Ghana 1,641, Afrika Kusini 1,615.

Mwaka 1978 China ilianza kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji , matunda ya juhudi za kukuza uchumi na kuondoa umaskini yanaonekana wazi. Mnamo mwaka 2010, Pato la Taifa la China (GDP) lilizidi Japani na kuwa uchumi wa pili kwa ukubwa duniani. Ifikapo mwaka 2019, Pato la Taifa la kila mtu la

China limeongezeka kufikia dola za Kimarekani 10,276. Mapema mwaka 2021 Rais wa China Xi Jinping alitangaza kuwa serikali imefanikiwa kuondoa watu wote katika umaskini uliokithiri, ikiwa ni mbele ya ratiba iliowekwa.

Sasa nchi nyingi za Afrika zimeanza kuona kuwa mfumo wa China wa kupata maendeleo na kukabiliana na umaskini unafaa zaidi.

Mafanikio ya kipekee ya kiuchumi na kisiasa ya China yanaweza kutajwa kama muujiza wa Wachina ambayo nchi za Kiafrika zina mengi ya kujifunza, anasema katibu mkuu wa chama tawala nchini Kenya cha Jubilee Raphael Tuju.

Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Ufuatiliaji na Utafiti wa Sera nchini Zambia Bernadette Deka-Zulu, anasema sera ya serikali ya China ya kuwapa kipaumbele wananchi kwenye mipango yake ya maendeleo ndio imesaidia pakubwa kuondoa umaskini.

“Haishangazi kwamba China imeweza kuwaondoa mamia ya mamilioni ya wakazi wake wa vijijini kutoka kwa umaskini kutokana na njia ya maendeleo ambayo inaweka watu mbele”, anasema Deka-Zulu.

CPC imekuwa injini ya maendeleo na mafanikio ya kutokomeza umaskini. Kwa sasa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kimetimiza miaka mia moja tangu kibuniwe.

Kwa viongoni na watu wa China CPC imekuwa ni kama gari la kusafirisha ndoto zao za maendeleo na mafanikio ya jamii yenye ustawi na hatma ya pamoja mwaka hadi mwaka.

Kwa chama kimoja kutimiza miaka 72 kwenye uongozi wa taifa pia ni muujiza mwingine. Lakini muujiza huo Raphael Tuju anasema, haungewezekana bila kuwepo na nidhamu.

“Lazima utoe sifa kwa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kwa kufanikiwa kuongoza nchi kwa nidhamu na kwa umakini ambazo zimewawezesha kufanikisha muujiza wa Wachina,” anasema Tuju.

Akibainisha njia bora ambayo China inakuza uchumi wake, anasema kuwa kuna mengi ambayo Afrika inaweza kujifunza kutoka kwa "muujiza wa Wachina, mojawapo ni kuwa na nidhamu kama ilivyo ndani ya CPC.

Kenya pia inaweza kujifunza kutokana na mafanikio ya China katika kupunguza umaskini. “Hakuna mfano katika historia ya ulimwengu ambapo watu wengi wameondolewa kwenye umasikini ndani ya muda mfupi kama vile tumeona nchini China,” anasema.

Hata hivyo anasema mchakato wa kujifunza na kufanikiwa ni mrefu. “Ufanisi hauwezi kupatikana mara moja. Tunajifunza kutoka kwa baadhi ya mifumo ambayo tulishuhudia wakati tulipotembelea China,” anasema Tuju.

CPC pia imekuwa dhabiti katika kuadhibu wanaohusika na ufisadi bila kujali vyeo au ngazi kwenye serikali.

Maofisa wa juu kwenye chama wanaohusika na ufisadi wanashatikwa kwa mujibu wa sheria, hali inayoongeza imani ya wananchi katika CPC.

Deka-Zulu anapongeza jukumu muhimu la Chama cha Kikomunisti cha China katika kupambana na rushwa na athari zake katika ajenda ya maendeleo ya China, na kuongeza kuwa juhudi za vita dhidi ya ufisadi kwa mikoa yote pia kumehakikisha kuwa maendeleo yanafika sehemu kamili zinazolengwa.

Mafanikio ya China yamesambaa kote duniani kimkakati Mwaka 2020 Kituo cha Uchumi na Utafiti wa Biashara cha Uingereza ambacho kinatoa ushauri wa uchumi kilitangaza kuwa uchumi wa China unatarajiwa kuwa mkubwa zaidi duniani ifikapo mwaka 2028.

Ufanisi huo wa kiuchumi unamaanisha kuwa jukumu la China kwenye maswala ya dunia pia yataongezeka.

Lakini mbele ya kufikia mwaka 2028 tayari ukuaji wa haraka wa kiuchumi wa China umeleta matumaini ya ukuaji wa hatma ya pamoja kwa kusaidia nchi nyingi barani Afrika kukuza uchumi wao.

Chini ya miradi ya Ukanda Mmoja na Njia Moja (BRI) ilioanzishwa mwaka 2013 nchi nyingi zimepata miradi inayotekelezwa kwa mikopo nafuu kutoka China kama vile reli, bandari na viwanja vya ndege.

Miundo mbinu yote hiyo inaendana na mahitaji halisi ya nchi za Afrika ili kuzisaidia kukuza biashara, uunganishaji na uchumi.

Cavince Adhere, mtaalam wa uhusiano wa kimataifa anasema Mpango wa Ukanda Mmoja na Njia Moja kama chombo bora cha kuchochea maendeleo ya pamoja kote duniani.

Anasema kuwa nguzo muhimu za BRI ikiwa ni pamoja na uratibu wa sera, maendeleo ya miundombinu, uwezeshaji wa biashara na ubadilishanaji wa watu kwa watu zinaleta picha kamili ya ushiriki wa moja kwa moja wa China kwenye maswala ya dunia.

“Nimefurahi kuona kuwa China sasa inapendekeza njia mpya za utekelezaji wa Mpango wa Ukanda Mmoja na Njia Moja kama ujenzi wa ushirikiano ikimaanisha kuwa nchi zinazoshiriki lazima ziwe na maoni, habari na kuchangia fedha, katika utekelezaji wa mradi huu,” anasema Adhere.

Kwa kuzingatia miradi hiyo ya BRI na mabadilishano ya mara kwa mara kati ya maafisa wa serikali za Afrika na China sasa ni wazi kuwa mwanya wa kufikia hatma ya pamoja ya binadamu utaendelea kupungua siku hadi siku.

CRI

  • Tags

You can share this post!

DIMBA: Mkenya anayetamba Uswidi kwa ueledi wake katika...

Watatoboa siasani?