• Nairobi
  • Last Updated December 4th, 2023 8:09 PM
Dkt Neema Lema atumia teknolojia kutibu watoto kwa kuwapa wazazi wao maelezo muhimu

Dkt Neema Lema atumia teknolojia kutibu watoto kwa kuwapa wazazi wao maelezo muhimu

NA MAGDALENE WANJA

WAKATI mwingine, kutibu mtoto mgonjwa huhitaji tu ushauri wa daktari.

Baadhi ya wagonjwa pia hawana uwezo wa kusafiri hadi hospitalini kutafuta matibabu kutokana na changamoto mbalimbali.

Dkt Neema Lema ambaye ni mtaalam wa watoto. Anatumia teknolojia ya Virtual Clinic kuwasaidia wazazi katika kuwatibu watoto. PICHA | MAGDALENE WANJA

Hii imerahisishwa na baadhi ya wataalamu wa afya ambao wamegundua mbinu ya kuwasiliana na mzazi kupitia video na kubaini maradhi.

Dkt Neema Lema ni mmojawapo wa wataalam wanaokumbatia teknolojia ya kisasa. Aidha, walianza mfumo huu wakati wa janga la Covid-19.

Dkt Neema Lema ambaye ni mtaalam wa watoto. Anatumia teknolojia ya Virtual Clinic kuwasaidia wazazi katika kuwatibu watoto. PICHA | MAGDALENE WANJA

Kwa kawaida, alikuwa akikutana na wagonjwa katika kliniki tatu ambazo alizifanyia kazi, ila kupitia video, wazazi hawakuhitajika kutoka majumbani mwao kutafuta matibabu.

Dkt Lema alizaliwa nchini Tanzania na baada ya kumaliza masomo yake, alihamia nchini Kenya ambako alianzisha familia mnamo mwaka 2012.

Mnamo mwaka 2016, alifungua ukurasa wa Facebook mahususi kumsaidia kuwasiliana na wagonjwa kwa kutia maelezo na vidokezo muhimu vya jinsi ya kuwatunza watoto wadogo na kutibu baadhi ya maradhi.

Dkt Neema Lema ambaye ni mtaalam wa watoto. Anatumia teknolojia ya Virtual Clinic kuwasaidia wazazi katika kuwatibu watoto. PICHA | MAGDALENE WANJA

Huduma ambazo hufanyika kupitia njia hii ni pamoja na utoaji ushauri (consultation).

“Baada ya ushauri, huwa ninamuelezea mzazi dawa anazohijika kuzinunua, na iwapo Kuna haja kufanya vipimo, mzazi Ana ruhusa kufanya vipimo katika maabara iliyo karibu naye,” alisema Dkt Lema.

Malipo ya huduma zake hufanya kupitia njia mbalimbali ikiwemo bima.

“Ijapokuwa huduma hii ina mapungufu yake, uvumbuzi wa aina hii ya teknolojia umesaidia sana katika kupunguza gharama za matibabu,” anaongeza.

Anabainisha kwamba huduma hii huwa na matokeo mema zaidi wakati mgonjwa anahitaji huduma zilizo za dharura au amepokea huduma kama hii hapo awali.

  • Tags

You can share this post!

Mkahawa Solutions: Programu inayorahisisha biashara...

Biashara za hoteli, gesti zanoga Mokowe miaka mitatu baada...

T L