• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 5:50 AM
Vyakula vya kuepuka kama una ngozi ya mafuta

Vyakula vya kuepuka kama una ngozi ya mafuta

Na MARGARET MAINA

IPO kauli iliyozoeleka ya “wewe ni kile unachokila”.

Bila shaka msemo huu hauna dosari yoyote. Inajulikana ukila vyakula vibaya vinaharibu mwili wako na hata ngozi hasa ngozi ya mafuta. Sio tu vinazidi kufanya ngozi yako kuwa na mafuta lakini pia vinaweza kusababisha matatizo ya ngozi kama chunusi, vichwa vyeupe na vyeusi na kadhalika.

Lakini habari nzuri ni kwamba unaweza kuepuka haya yote kama utaondoa baadhi ya vyakula katika mlo wako.

Hivi ni baadhi ya vyakula ambavyo unatakiwa kukaa mbali navyo kama ngozi yako ni ya mafuta.

Vyakula venye au vilivyotengenezwa na maziwa mengi

Vinaweza vikawa ni vyakula vyako pendwa au vina ulazima kutumika katika maandalizi ya chakula lakini tuamini hivi vyakula vina matokeo ‘mabaya’ ambayo yanaongeza mafuta katika ngozi yako. Unaweza kupunguza au kuacha kabisa kutumia vyakula kama ice cream, siagi na kadhalika.

Kahawa au chai

Kahawa na chai humaliza maji mwilini na hii inaweza kusababisha uzalishaji wa mafuta na kusababisha chunusi na vipele vidogovidogo. Unaweza kupunguza kunywa chai na kahawa na kunywa maji mengi na sharubati ya kujitengenezea.

Pombe

Pombe ni kama kahawa ina maliza maji mwailini.Hii inaweza kupelekea uzalishaji wa mafuta mwilini na kusababisha ngozi kuendelea kuwa na mafuta lakini pia kupata matatizo ya ngozi kama vile chunusi.

Sukari

Kutumia sukari husababisha kupanda katika viwango wa sukari iliyo kwenye damu. Hii inaongoza kwa uzalishaji wa insulini zaidi, ambayo, kwa upande wake, husababisha tezi za kuzalisha mafuta zaidi. Inasababisha mtu awe na ngozi yenye mafuta ambayo matokeo yake huleta chunusi. Epuka kula mikate, jamu, vyakula vya unga, na kadhalika. Tumia sukari ya asili kama iliyo kwenye matunda na mboga, kwa kiasi.

Chumvi

Chumvi ya ziada inaweza kusababisha uhifadhi wa maji na kuvimba. Inaweza pia kusababisha ongezeko la mafuta katika ngozi pale ambapo mwili unajaribu kupambana na maji machafu yanayosababishwa na matumizi makubwa ya chumvi. Epuka kula chumvi ya ziada au vyakula vyenye chumvi nyingi.

  • Tags

You can share this post!

Chanjo ya lazima kwa watumishi wa umma

Serikali yataka walimu warudishe ‘karo’ haramu