• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 11:59 AM
Aliyekuwa kapteni wa Colombia, Freddy Rincon, aaga dunia kwenye ajali ya barabarani

Aliyekuwa kapteni wa Colombia, Freddy Rincon, aaga dunia kwenye ajali ya barabarani

Na MASHIRIKA

NAHODHA wa zamani wa timu ya taifa ya Colombia, Freddy Rincon, ameaga dunia baada ya kupata majeraha mabaya ya kichwa kutokana na ajali ya barabarani.

Gari dogo lililokuwa likiendeshwa na nyota huyo mwenye umri wa miaka 55 liligongana na basi mnamo Aprili 11, 2022 mjini Cali, Colombia. Rincon ambaye pia aliwahi kuchezea Real Madrid ya Uhispania, alifungia Colombia mabao 17 kimataifa na akawa sehemu ya kikosi kilichotegemewa kwenye fainali za Kombe la Dunia za 1990, 1994 na 1998.

Kwa pamoja na Carlos Valderrama, anashikilia rekodi ya kuwakilisha Colombia kwenye idadi kubwa zaidi ya mechi za Kombe la Dunia (10). Rincon alikuwa sehemu ya kikosi kilichomaliza subira ya miaka 28 ya Colombia kunogesha Kombe la Dunia baada ya kuongoza timu yake ya taifa kuingia fainali za 1990 nchini 1990.

Alifunga bao katika sare ya 1-1 dhidi ya West Germany walioishia kuwa wafalme wa dunia kwenye mojawapo ya mechi za fainali hizo. Rincon aliwahi pia kuvalia jezi za klabu za Napoli, Palmeiras na Santos kabla ya kuongoza Corinthians kunyanyua taji la Kombe la Dunia kwa klabu mnamo 2000.

You can share this post!

Man-City sasa kuvaana na Real kwenye nusu-fainali ya UEFA

Kocha Erik Ten Hag wa Ajax kupokezwa na Man-United mkataba...

T L