• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 5:50 AM
Colombia wapepeta Ecuador 1-0 kwenye pambano la kuwania taji la Copa America

Colombia wapepeta Ecuador 1-0 kwenye pambano la kuwania taji la Copa America

Na MASHIRIKA

COLOMBIA sasa wanashikilia nafasi ya pili nyuma ya mabingwa watetezi Brazil katika msimamo wa Kundi A kwenye Copa America baada ya kupepeta Ecuador 1-0 katika mchuano wao wa kwanza mjini Cuiaba, Brazil.

Goli hilo la pekee na la ushindi kwa upande wa Colombia lilifumwa wavuni na Edwin Cardona mwishoni mwa kipindi cha kwanza.

Kikosi hicho sasa kitavaana na Venezuela katika mechi ya pili mnamo Juni 17 usiku huku Brazil waliokomoa Venezuela 3-0 katika mchuano wao wa kwanza kundini wakishuka dimbani kumenyana na Peru siku hiyo.

Colombia walishuka dimbani kuvaana na Ecuador wakipania kuendeleza ubabe uliowavunia ushindi wa 3-0 dhidi ya Peru na sare ya 2-2 dhidi ya Argentina katika mechi mbili zilizopita za kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia za 2022 nchini Qatar.

Brazil walipokezwa idhini ya kuwa wenyeji wa Copa America mwaka huu baada ya maandamano ya raia dhidi ya serikali kuzuka nchini Colombia na maambukizi ya virusi vya corona kuzidi nchini Argentina.

Colombia na Argentina ndio waliokuwa wawe waandalizi wa pamoja wa fainali za Copa America mwaka huu wa 2021 na hiyo ingekuwa mara ya kwanza tangu 1916 kwa fainali hizo kuandaliwa na mataifa mawili.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Slovakia washangaza Poland kwa kuipokeza kichapo cha 2-1...

Hadhi: Wito serikali iimarishe majukwaa ya kazi za sanaa...