• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:35 AM
Japan wapepeta Mexico na kuendeleza ubabe wao kwenye Olimpiki

Japan wapepeta Mexico na kuendeleza ubabe wao kwenye Olimpiki

Na MASHIRIKA

WENYEJI Japan waliwakomoa Mexico 2-1 mnamo Jumapili jijini Tokyo na kusajili ushindi wao wa pili kwenye Olimpiki zinazoendelea.

Mabao ya Japan yalifungwa na Takefusa Kubo na Ritsu Doan.

Japan ambao kwa sasa wanaselelea kileleni mwa Kundi A kwa alama sita, walishuka ulingoni wakijivunia kucharaza Afrika Kusini 1-0 katika mechi ya awali.

Katika Kundi B, Mikel Oyarzabal wa Real Sociedad katika Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) alisaidia Uhispania kupepeta Australia 1-0 siku tatu baada ya kulazimishiwa sare tasa na Misri.

Ujerumani waliopokezwa kichapo cha 4-2 kutoka kwa mabingwa watetezi Brazil katika mechi ya kwanza, walijinyanyua na kuwakung’uta Saudi Arabia 3-2 katika Kundi D.

Katika Kundi C, fowadi Chris Wood wa Burnley aliwachochea New Zealand kucharaza Honduras 3-2 huku Korea Kusini wakiwaponda Romania 4-0.

MATOKEO YA OLIMPIKI (Jumapili):

Ufaransa 4-3 Afrika Kusini

Japan 2-1 Mexico

New Zealand 2-3 Honduras

Romania 0-4 Korea Kusini

Misri 0-1 Argentina

Australia 0-1 Uhispania

Brazil 0-0 Ivory Coast

Saudi Arabia 2-3 Ujerumani

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Raila ataja sera atakayofuata akiibuka mshindi mwaka 2022

Washirika wa Kalonzo wapuuza hatua ya Kibwana