• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 2:29 PM
Mashabiki 500 wa klabu za ugenini kuhudhuria mechi

Mashabiki 500 wa klabu za ugenini kuhudhuria mechi

Na MASHIRIKA

MASHABIKI wa vikosi vitakavyokuwa vikichezea ugenini katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) watakubaliwa kuhudhuria mechi mbili za mwisho katika kampeni za msimu huu baada ya serikali kulegeza baadhi ya kanuni za kudhibiti maambukizi ya Covid-19.

Ni mashabiki wa nyumbani pekee ndio waliowahi kukubaliwa kuingia uwanjani kuhudhuria mechi za EPL tangu janga la corona lilipozuka mwishoni mwa Disemba 2019.

Sasa huenda jumla ya mashabiki 500 wa ugenini wakapewa idhini ya kuhudhuria mechi mbili za mwisho za vikosi vyao mnamo Mei mwaka huu.

Vinara wa EPL pia wamelazimika kuhamishia mechi zote za raundi ya 37 hadi katikati ya wiki, yaani Mei 18-19 ili kuhakikisha kwamba kila kikosi kina mchuano mmoja wa nyumbani utakaohudhuriwa na mashabiki wao kabla ya kipenga cha kuashiria mwisho wa kampeni za msimu huu kupulizwa rasmi.

Aidha, kuanzia Mei 17, kumbi za michezo mbalimbali nchini Uingereza itakuwa huru kuruhusu mahudhurio ya hadi mashabiki 10,000 au asilimia 25 ya mashabiki – kutegemea ni idadi gani itakuwa ndogo zaidi.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

GWIJI WA WIKI: Mhadhiri, mkalimani na mtafsiri...

Leicester City wala sare dhidi ya Southampton