• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 1:20 PM
Ni mashabiki 40 pekee wataruhusiwa kushuhudia mechi

Ni mashabiki 40 pekee wataruhusiwa kushuhudia mechi

NA ABDULRAHMAN SHERIFF

MASHABIKI 40 pekee ndio watakaoruhusiwa kushuhudia kila mechi za Ligi ya Taifa Daraja la Pili Kanda ya Kaskazini inayotarajia kuanza rasmi Jumamosi Februari 6, 2021.

Ni wapenda soka 40 pekee katika kila mechi, 20 kutoka kila timu ambazo zitakuwa zikipambana uwanjani ndio watakaoruhusiwa kushuhudia mechi za timu zao mbili.

Katibu wa FKF wa kanda hiyo, Lilian Nandundu amesema timu zitakazokutana katika mechi zitahitajika kuwasilisha majina ya mashabiki wao 20 wakati wa kufanyika kwa mkutano wa kujadiliana juu ya mechi hiyo.

“Ni viwanja vile pekee vitakavyokuwa na kuta ndizo zitakazoruhusiwa kutumika kwa mechi za ligi hii,” akasema Lilian ambaye alisisitiza kuwa timu za nyumbani ndizo zitahitajika kuchora alama kwenye viwanja vitakavyotumika kwa mechi.

Alieleza kuwa timu zitakazokutana ndizo zitakazohitajika kutoa Sh5,000 kila moja wakati wa mkutano wa matayarisho ya mechi utakapofanyika na timu ya nyumbani itahitajika kuweka walinda usalama japo wawili wenye kujihami kwa silaha.

Klabu ya nyumbani itahitajika kuweka gari la ambulensi ama gari lolote ambalo litaweza kutumika kukitokea udhru na kuwe na akiba ya hospitali iliyo karibu na uwanjani. Timu yoyote itakayoshindwa kucheza mechi tatu, itabanduliwa nje ya ligi hiyo.

Timu za nyumbani zitahitajika kuweka watoto wa kuokota mipira nyakati za mechi zao na wawe na mipira isiyopungua minne. Timu yoyote inayotaka kuahirisha mechi, ni lazima wawasilishe masaa 72 kabla ya mechi kuchezwa.

  • Tags

You can share this post!

Klabu 19 kupigania taji la Ligi ya Taifa Daraja la Pili...

Shujaa, Lionesses wapata motisha ya Sh2.8 milioni kuenda...