• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 11:36 AM
Okutoyi arejea nyumbani baada ya jeraha

Okutoyi arejea nyumbani baada ya jeraha

Na GEOFFREY ANENE

NYOTA Angella Okutoyi amerejea nchini Jumamosi kutoka Tunisia baada ya kulazimika kujiondoa kutoka mashindano ya tenisi ya malipo ya W15 Monastir kwa sababu ya jeraha la bega na mkono.

Malkia huyo wa Afrika wa mashindano ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 18, aliumia dhidi ya Tanuchaporn Yongmod,22, kutoka Thailand katika mechi ya kuingia raundi ya 32-bora mnamo Desemba 5 mjini Monastir. Alilenga kushiriki mashindano matatu ya W15 Monastir mnamo Desemba 6-12, Desemba 13-19 na Desemba 20-26.

Hata hivyo, ameamua kurejea nyumbani kujipanga kwa mwaka 2022 anapoendelea kupata afueni. Okutoyi, 17, alikuwa narejea kwenye mashindano ya tenisi ya malipo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2019 alipobanduliwa katika raundi ya 16-bora jijini Nairobi.

Anashikilia nafasi ya 1,228 kwenye viwango bora vya Shirikisho la Tenisi Duniani (ITF) vya tenisi ya watu wazima baada ya kuaga mapema mashindano ya kwanza ya W15 Monastir. Katika tenisi ya chipukizi, Okutoyi ni nambari 94 baada ya kuteremka nafasi moja Desemba 6.

You can share this post!

Wasimamizi waelezea hatua ilizopiga MKU katika utoaji...

Kiongozi wa upinzani Benin akamatwa kwa tuhuma za ugaidi

T L