• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 9:16 PM
Kiongozi wa upinzani Benin akamatwa kwa tuhuma za ugaidi

Kiongozi wa upinzani Benin akamatwa kwa tuhuma za ugaidi

Na AFP

PORTO-NOVO, Benin

KIONGOZI wa upinzani nchini Benin na waziri wa zamani wa haki Reckya Madougou jana alihukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani kwa tuhuma za ugaidi.

Hukumu hiyo ilitolewa katika makakama maalum jijini Porto-Novo.Baada ya kesi hiyo kusikizwa kwa zaidi ya saa 20, Madougou, 47, alipatikana na hatia kwa kosa la “kushiriki vitendo vya ugaidi” na mahakama hiyo ya kushughulikia kesi za ugaidi na uhalifu wa kiuchumi.

Mnamo Jumanne mahakama hiyo pia ilimhukumu mwanasiasa mwingine wa upinzani miaka 10 gerezani. Wakosoaji wanasema mahakama hiyo iliyoanzishwa 2016 imekuwa ikitumiwa na utawala wa Rais Patrice Talon kuwaandama viongozi wa upinzani na kuelekeza Benin katika utawala wa kidekteta.

“Mahakama hii imeamua, kimakusudi, kuadhibu mtu asiye na hatia”, Madougou akasema muda mfupi baada ya hukumu dhidi yake kusomwa. “Sijawahi na sitawahi kuwa gaidi,” akaongeza.

Naye Robert Dossou, ambaye ni mmoja mawakili wa Madougou, akasema: “Hii ni siku ya huzuni kwa utekelezaji wa haki, nashikilia kuwa hakuna ushahidi kwamba nimehusishwa na ugaidi” Madougou ni mmoja wa viongozi wa upinzani nchini Benin ambao wamepigwa marufuku kushiriki katika uchaguzi uliofanyika Aprili.

Talon alishinda kwa kupata asilimia 86 za kura na kupata nafasi ya kuendelea kuongoza muhula wa pili. Alikamatwa mnamo Machi mwaka huu, wiki kadhaa kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo. Alikabiliwa na tuhuma za kufadhili mipango ya mauaji ya wanasiasa ili kuhujumu uchaguzi na hatimaye kusababisha msukosuko nchini humo.

You can share this post!

Okutoyi arejea nyumbani baada ya jeraha

Blak Blad yaosha Homeboyz raga ya Kenya Cup

T L