Felix na Suarez waibeba Atletico dhidi ya Valencia ligini

Na MASHIRIKA

JOAO Felix na Luis Suarez walisaidia waajiri wao – Atletico Madrid – kutoka nyuma na kuwapokeza Valencia kichapo cha 3-1 katika mechi ya Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) mnamo Januari 24.

Valencia walitangulia kuliona lango la wenyeji katika dakika ya 11 kupitia kwa Uros Racic kabla ya Atletico ambao ni viongozi wa jedwali kusawazishiwa na Felix kunako dakika ya 23.

Felix alichangia bao la pili ambalo Atletico walifungiwa na Suarez mwanzoni mwa kipindi cha pili kabla ya Angel Correa kutokea benchi na kupachika wavuni bao la tatu lililowapa miamba hao wa soka ya Uhispania ushindi wa saba mfululizo ligini.

Chini ya kocha Diego Simeone, Atletico kwa sasa wanaselelea kileleni mwa jedwali la La Liga kwa alama 47, saba zaidi kuliko mabingwa watetezi Real Madrid.

MATOKEO YA LA LIGA (Januari 24):

Elche 0-2 Barcelona

Atletico 3-1 Valencia

Osasuna 3-1 Granada

Celta Vigo 1-1 Eibar