• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 6:55 AM
‘Wazazi wetu walikuwa marafiki na ndio maana mimi na Rais huitana ndugu’

‘Wazazi wetu walikuwa marafiki na ndio maana mimi na Rais huitana ndugu’

Na SAMMY WAWERU

Kinara wa chama cha ODM Bw Raila Odinga amesema usahibu wake na Rais Uhuru Kenyatta haukuanza baada ya salamu za maridhiano mnamo Machi 2018, maarufu kama handisheki.

Bw Odinga Alhamisi alisema undugu kati yake na Rais Kenyatta ulianza kitambo.

Akihojiwa na kituo cha redio cha Inooro na Inooro TV, vinavyopeperusha matangazo yake kwa lugha ya Kikuyu, Bw Odinga alisema babake Mzee Jaramogi Oginga Odinga na Mzee Jomo Kenyatta (baba ya Rais Kenyatta) walikuwa marafiki.

“Urafiki wangu na Rais Kenyatta haukuanza 2018, ni wa tangu zamani. Mzee Jomo Kenyatta alikuwa akitembea eneo la Kisumu. Wazazi wetu walikuwa marafiki na ndio maana mimi na Rais huitana ndugu,” akasema.

Mzee Jaramogi aliwahi kuhudumu kama makamu wa Rais wa Mzee Kenyatta.

Kulingana na Bw Odinga, salamu za maridhiano ziliashiria kuweka kando tofauti za kisiasa kati yake na Rais, ila hawakuwa mahasimu.

“Tuliamua kuunganisha nchi kutokana na machafuko yaliyoshuhudiwa katika uchaguzi mkuu wa 2017,” kiongozi huyo wa ODM akasema, akielezea yaliyojiri.

Bw Odinga aliwania kiti cha urais akisaidiwa na mgombea mwenza Kalonzo Musyoki, na ambaye ni kiongozi wa chama cha Wiper.

Rais Kenyatta (Jubilee) aliwania kuhifadhi kiti chake, Naibu wa Rais William Ruto akiwa mgombea mwenza.

You can share this post!

Ujenzi wa bandari Kwale kuendelea

Barcelona waponea kuondolewa na Granada kwenye Copa del Rey