• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Sofapaka kuwa na kikosi kamili dhidi ya Bidco United

Sofapaka kuwa na kikosi kamili dhidi ya Bidco United

NA ABDULRAHMAN SHERIFF

SOFAPAKA FC inatarajia kuwa na wachezaji wake wote watatu wanaochezea timu za taifa za Kenya na Burundi itakapokutana na Bidco United FC kwenye mechi ya Ligi Kuu ya FKF itakayochezwa uwanja wa Dawson Mwanyumba mjini Wundanyi siku ya Jumapili.

Meneja wa Sofapaka FC, Hilary Echesa amesema wanaendelea kujitayarisha kwa mechi hiyo na watakuwa na wanasoka wao wawili wa Harambee Stars, beki Michael Kibwage na kiungo Lawrence Juma na kiungo Mburundi Amissi Bizimana katika mchezo huo.

Echesa anasema golikipa wao aliyeumia bega wakati wa mechi yao na KCB, Mubarak Aigba ameshapona na huenda akawa miongoni mwa wachezaji watakaokuwako katika kikosi cha kukabiliana na Bidco United.

Kuhusu matayarisho ya mechi yao hiyo, Echesa amesema wanajitahidi kunyakuwa pointi zote tatu kwani wanahitaji kupanda ngazi na kuwa katika nafasi nzuri ili wapate kushindana na walio kileleni mwa jedwali la ligi hiyo. “Ligi bado iko changa na tunajitahidi tuwe hapo kileleni,” akasema.

Mashabiki wa soka wa Wundanyi na maeneo mengine ya Kaunti ya Taita Taveta wameendelea kutoa ombi kwa serikali ya Kenya kuwapa ruhusa mashabiki wa mchezo huo kukubaliwa kushuhudia mechi ili wapate kujiburudisha.

“Tunaomba serikali ituruhusu mashabiki kushuhudia mechi za soka kwani sisi hapa tuna hamu ya kuishuhudia na kuishangilia Sofapaka inayofunzwa na Ken Odhiambo ambayo imechagua uwanja wetu kwa wa mechi zao za nyumbani,” amesema shabiki wa soka wa Wundanyi, Gerald Maghanga.

Timu ya Sofapaka iko kwenye nafasi ya tisa ikiwa na pointi 18 kutokana na mechi 13 ilizocheza hakli wapinzani wao wa Bidco United waliocheza mechi 14 wana alama 20.

You can share this post!

Lengo ni kusalia kwa tano bora ligini – Mwatate FC

Kimani kuidhinishwa rasmi naibu kocha Bandari