• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Mahangaiko tele familia zilizofurushwa katika ardhi zao zikiishi shuleni

Mahangaiko tele familia zilizofurushwa katika ardhi zao zikiishi shuleni

Na George Munene

MAMIA ya familia zilizofurushwa kutoka nyumba zao eneo la Makina, Kaunti ya Embu wiki jana, sasa zinaishi kwenye makao ya muda katika shule mbalimbali eneo hilo.

Familia hizo zilitimuliwa kutoka ardhi ambayo umiliki wake umeibua utata, huku Mamlaka ya Mto Athi (TARDA) ikisisitiza ardhi hiyo ni yake.

Baada ya kufurushwa kwenye tukio lililopelekea kukamatwa kwa Mbunge wa Mbeere Kusini, Bw Geoffrey King’ang’i, familia hizo zimepata hifadhi ya muda katika shule za msingin za Ndunguni, Muthithu na Mwanyani.

Kwa sasa wanaishi katika hali mbaya huku wakililia msaada kutoka kwa wahisani na serikali kuu na kaunti.’Maisha ni magumu na yafaa tusaidiwe kabla njaa haijatuangamiza,’ akasema mmoja wa waathiriwa Elizabeth Muoki.

Bw King’ang’i naye alisema familia hizo zimejarundikana katika madarasa kutokana na idadi yao kubwa na ziko katika hatari ya kuambukizwa virusi vya corona.’

Hawana barakoa na sanitaiza kwa hivyo hali ikiendelea hivyo, wataambukizwa virusi vya corona,’ akasema mbunge huyo.

Alifichua kwamba ameongea na Waziri wa Usalama wa Ndani, Dkt Fred Matiang’i na katibu wa wizara hiyo, Dkt Karanja Kibicho ambao walimhakikishia kwamba familia hizo zitaruhusiwa kurejea katika nyumba zao zilizobomolewa na zisaidiwe kuzijenga upya.

 

You can share this post!

Ulipaji fidia kwa wakazi wa Lamu ni kabla ya Juni

Gavana hatarini kwa kumpa mkewe mamlaka ya kusimamia kaunti