• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Mumias: Wabunge wataka mrasimu atoe ripoti ya mapato

Mumias: Wabunge wataka mrasimu atoe ripoti ya mapato

Na BENSON AMADALA na SHABAN MAKOKHA

BAADHI ya wabunge kutoka Kaunti ya Kakamega wanataka ripoti kuhusiana na mapato ya kemikali ya ethanol inayotengenezwa katika kiwanda cha sukari cha Mumias.

Wabunge hao wanataka meneja mrasimu wa kiwanda hicho, Bw Pongangipalli Venkata Ramana Rao, kutoa ripoti ya kina kuhusiana na mapato hayo. Kiwanda hicho kimekwa kikikabiliwa na hali ngumu

Wabunge Benjamin Washiali (Mumias Mashariki), Peter Nabulindo (Matungu) na Ayub Savula (Lugari), walisema Bw Rao, aliyeteuliwa kama meneja mrasimu na Kenya Commercial Bank (KCB), anapaswa kutoa maelezo hayo anapojiandaa kukamilisha mchakato wa kukodisha kiwanda hicho kwa mwekezaji.

Bw Rao aliyeteuliwa kama meneja mrasimu na KCB mnamo Septemba 24, 2019, amekuwa akihusika na utengenezaji wa kemikali ya ethanol hadi kufikia Machi mwaka huu, katika harakati za kuimarisha mapato na kustawisha shughuli za kiwanda hicho.

Kampuni hiyo ilikuwa imesimamisha utengenezaji huo, kutokana na upungufu wa malighafi inayotumiwa kuzalisha kemikali hiyo.

Hata hivyo, wabunge hao wamedai kuwa meneja huyo hajajitahidi vilivyo kufufua kiwanda hicho.

You can share this post!

Vigogo wawania Mlima Kenya kama mpira wa kona

Pendekezo vyeti vya kuzaliwa vitumike kusajili wapigakura