• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Bunge la Uganda laandikisha visa 200 vya maambukizi ya corona ndani ya wiki 3

Bunge la Uganda laandikisha visa 200 vya maambukizi ya corona ndani ya wiki 3

Na Daily Monitor

Tafsiri: CHARLES WASONGA

ZAIDI ya wafanyakazi 200 wa Bunge la Uganda, wakiwemo wabunge, wamepatikana na virusi vya corona ndani ya kipindi cha wiki tatu zilizopita.

Habari hizo zinajiri wakati ambapo kuna hofu kwamba madereva wa wabunge na jamaa zao pia wameambukizwa ugonjwa huo ambao umeua zaidi ya watu 700 nchini humo.

Duru ziliambia “Daily Monitor” kwamba vipimo vya hivi punde vilivyofanywa katika bunge hilo vilionyesha kuwa kuna maambukizi mapya yanayonakiliwa kila siku.Wabunge wote na wafanyakazi waliopatikana na virusi vya corona walishauriwa kujitenga na kutafuta matibabu kwa dharura katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Makerere.

Wengine ambao waliokuwa wakionyesha dalili za kuambukizwa ugonjwa huo walifanyiwa uchunguzi katika maabara fulani iliyoko eneo la Butika.Baadhi ya idara zilizoathiriwa zaidi na Covid-19 katika bunge la Uganda ni; Ununuzi bidhaa, Fedha, Habari, Mawasiliano na Teknolojia na Afisi ya Mlinzi.

Ili kuzuia uwezekano wa kuenea kwa virusi hivyo zaidi Spika Jacob Oulanyah aliamuru kufungwa kwa bunge hilo kwa kipindi cha majuma mawili.Naibu karani wa bunge Henry Wasswa Yoweri aliwaandikia wabunge akiwajuza kuhusu kufungwa kwa majengo ya bunge ili kuzuia kusambaa kwa Covid-19.

“Bunge la Uganda, sawa na maeneo mengine ya nchini, limeathiriwa na wimbi la pili la janga la corona. Taifa limeandikisha kiwango cha maambukizi cha asilimia 17.1,” akasema Wasswa.

“Ili kuzuia maambukizi ya Covid-19, usimamizi wa bunge kwa ushauriano na afisi ya Spika imefungwa bunge kwa wiki mbili ili kutoa nafasi kwa unyunyiziaji dawa za kuua wadudu katika majengo yote,” akaongeza.

 

  • Tags

You can share this post!

Shule zakataa amri ya KNEC kuhusu mtihani

Ilani kwa wahudumu wa matatu kuhusu ukiukaji wa sheria...