• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 7:47 PM
Chanjo: Rais aondoa hofu kuhusu AstraZeneca

Chanjo: Rais aondoa hofu kuhusu AstraZeneca

Na WANDERI KAMAU

RAIS Uhuru Kenyatta, Ijumaa aliondoa tashwishi ambazo zimeibuka kuhusu chanjo aina ya AstraZeneca inayotumika nchini.

Rais akiwahakikishia Wakenya kuwa serikali iko macho kuhusu hali zozote ambazo huenda zikatokea.

Hofu hiyo imeibuka miongoni mwa Wakenya baada ya nchi kadhaa za Ulaya kusimamisha utoaji wake.

Nchi hizo ni Denmark, Norway, Iceland, Austria, Estonia, Lithuania, Luxemborg, Italia na Latvia.

Mataifa hayo yalisimamisha chanjo hiyo baada ya watu kadhaa kulalamikia tatizo la mgando wa damu.

Afrika Kusini pia ilikuwa imesimamisha utoaji wa chanjo hiyo kwa muda, baada ya kuonekana kutokabili aina mpya ya virusi vya corona.

Lakini Ijumaa, Rais Kenyatta alisema taasisi husika za afya zinafuatilia kwa kina hali zozote ambazo huenda zikaibuka kuhusiana na chanjo hiyo.

“Hakuna tatizo ambalo limeibuka nchini kufikia sasa. Wahudumu wetu wa afya wako macho kuhakikisha watashughulikia suala lolote ambalo huenda likatokea miongoni mwa wale ambao tayari wamepewa,” akasema Rais.

Hilo linajiri huku baadhi ya Wakenya wakitoa hisa mseto kuhusu chanjo hizo.

Baadhi wameeleza hisia mseto kuhusu usalama wake, wakisema watachanjwa tu ikiwa viongozi watajitokeza kupewa hadharani.

Tangu shughuli hiyo kuanza, ni viongozi wachache ambazo wamejitokeza hadharani wengi wao wakiwa ni magavana.

Rais alisema chanjo hiyo inatolewa kwa hiari ya mtu binafsi.

You can share this post!

Nyanya aomba mahakama isimwachilie mwanawe jela

Watanzania waulizia aliko rais huku serikali ikinyamaza